· Juni, 2009

Habari kuhusu Iran kutoka Juni, 2009

Iran: Video za Maandamano ya Upinzani Zazidi Kumiminika

  17 Juni 2009

Zaidi ya watu 100,000 waliandamana mjini Tehran Jumatatu iliyopita ili kumuunga mkono mgombea urais mwanamageuzi, Mir Hussein Mousavi pamoja na madai yake ya kuataka kubatilishwa kwa matokeo ya uchaguzi ambayo yalimtangaza rais aliye madarakani Mahmoud Ahmadinejad kama mshindi katika uchaguzi wa tarehe 12 Juni. Damu ilimwagika mwishoni mwa maandamano hayo. Watu wapatao 7 walipoteza maisha yao.

Irani: Maandamano na Ukandamizaji

  16 Juni 2009

Mamia ya maelfu ya Wairani mjini Tehran na katika miji mingine kadhaa wameandamana kumuunga mkono mgombea urais Mir Husein Mousavi huku wakiipuuza amri ya serikali inayokataza maandamano. Japokuwa huduma za Twita, FaceBook pamoja na YouTube zimezuiliwa kwa kuzimwa nchini Iran, Wairani wengi wamekuwa wakitumia tovuti-vivuli ili kuvizunguka vichujio vilivyowekwa na wanaripoti habari kadiri zinavyotokea. Utawala wa Irani pia umezuia huduma za jumbe za maandishi kwa kutumia simu za mkononi (SMS), kadhalika utawala huo unachuja tovuti kadhaa zinazoakisi maoni ya wanamageuzi.

Irani: Kimbunga cha Maandamano Baada Ya Uchaguzi

  14 Juni 2009

Maelfu ya watu waliandamana mjini Tehran, Mashdad na kwenye miji mingine mikubwa ya Irani ili kupinga ushindi wa Rais Mahmoud Ahmadinejad katika uchaguzi mkuu uliofanyika Ijumaa. Washindani wawili wanamageuzi pamoja na mashabiki wao wanasisitiza kwamba palitokea udanganyifu.

Uchaguzi Wa Irani Katika Picha

  13 Juni 2009

Uchaguzi wa rais nchini Irani utafanyika tarehe 12 Juni. Ni watu wanne tu kati ya watu zaidi ya 400 waliojiandikisha ambao wamepewa idhini rasmi na Baraza la Walezi kuwa wagombea katika uchaguzi. Macho makali ya wanablogu-wapiga picha yamenasa nyakati na taswira katika mitaa ya Irani ambako watu walikuwa wakiwapigia debe wagombea wanaowapenda.