· Novemba, 2013

Habari kuhusu Misri kutoka Novemba, 2013

Udadisi wa Sami Anan

  15 Novemba 2013

Mwanablogu wa Misri Zeinobia anatoa maoni yake machache kuhusu kuibuka tena kwa Sami Anan, Mnadhimu mkuu wa zamani wa Majeshi ya Misri. Je, ana mpango wa kugombea urais? Mwanahabari wa Sauti za Dunia Mtandaoni Victor Salama anasimulia zaidi.

Misri: “Morsi Hatarudi Madarakani”

  14 Novemba 2013

Aliyekuwa rais wa Misri Mohamed Morsi hatarudi madarakani, anasema mwanablogu wa Misri Alya Gadi, kwenye mtandao wa Twita. Kuufanya ujumbe wake wazi, ametafsiri kwa lugha mbalimbali: مرسي لن يعود – Morsi is not coming back – Morsi no va a volver – Morsi ne reviendra pas – Morsi kommt nicht zurück...

Misri katika Harakati za Kujitafutia Makazi

  12 Novemba 2013

Ni wapi mtu hujisikia kuwa yupo nyumbani? mwanablogu wa Misri Tarek Shalaby atoa maoni yake: Baadhi ya watu wanasema kuwa nyumbani ni pale palipo na kitanda chake, wengine wanadai kuwa nyumbani ni pale unapoweza kupata mtandao huru wa intaneti. naweza kusema kuwa nyumbani ni pale ambapo mishahara yako imehamishiwa.

Misri: Sabuni ya Ubikira?

Mwanaharakati wa Kimsiri Nelly Ali anashangaa: Wakati #Misri iko bize…Upuuzi kama huu uko kwenye makabati yetu ukiharibu maisha yetu "Sabuni ya Ubikira"#wanawake/a> pic.twitter.com/IXplFn2kY7 — Nelly Ali (@nellyali) November 1, 2013 Wakati #Misri iko bize…Upuuzi kama huu uko kwenye makabati yetu ukiharibu maisha yetu Sabuni ya Ubikira Akimjibu, anamwambia: @nellyali imekuwa...