· Juni, 2013

Habari kuhusu Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini kutoka Juni, 2013

Wanaharakati 36 wa Azeri Wakamatwa nchini Iran

  29 Juni 2013

Wanaharakati thelathini na sita wa Azeri akiwamo mwanablogu mmoja, Kiaksar, walikamatwa siku ya Alhamisi, 27 Juni katika eneo la Urmia. Vikosi vya usalama viliwaachilia huru wanaharakati hao 300 baada ya kuwahoji kwa masaa kadhaa.

Maandamano ya Kudai Uhuru Yafanyika Kwenye Miji ya Saudi Arabia.

  16 Juni 2013

Makundi madogo madogo ya wanawake wa Saudi Arabia kwa wakati mmoja yaliitisha “mikutano ya kudai uhuru” katika maeneo mbalimbali ya majiji ya Saudi Arabia mnamo tarehe 10 Juni, 2013, maandamano yaliyoratibiwa na kundi lisilojulikana la mawakili @almonaseron [ Waungaji mkono] linaloshinikiza kuachiwa huru kwa ndugu zao wanaoshikil

Israeli: Waandamanaji Wakumbana na Ukatili wa Polisi Jijini Yerusalemu

  12 Juni 2013

Maandamano yaliyoandaliwa na vikundi vitatu vinavyohusiana na Vuguvugu la Israel la haki ya kijamii (#j14) yalifanyika jijini Yerusalemu mnamo Jumamosi usiku (Juni 8). Waandamanaji walidai kubatilishwa kwa uamuzi wa kuuza zaidi kiasi kikubwa cha hifadhi ya gesi wakati ni asilimia 12.5 tu ya mapato hayo yatakwenda serikalini kama kodi.

Misri: Wafanyakazi wa Asasi Zisizo za Kiserikali Nchini Misri Wafungwa Jela

  11 Juni 2013

Kuhukumiwa kwa wafanyakazi wa ki-Misri na kigeni wanaofanya kazi katika asasi zisizo za kiserikali (NGO) kifungo cha hadi miaka mitano jela, kumesababisha hasira katika mitandao ya kijamii na katika maeneo mengine. Hatua hiyo imeonekana kama onyo kwa mashirika ya kutetea haki za binadamu na yale yanayokuza demokrasia.

Iran: Utani Kuhusu Mdahalo wa Urais

  6 Juni 2013

Raia wa mtandaoni kadhaa walitwiti kuhusu mjadala wa pili wa rais na waliwakejeli wagombea. Potkin Azarmehr alitwiti “Wagombea urais wanaweza kuombwa kucheza muziki.”