· Aprili, 2013

Habari kuhusu Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini kutoka Aprili, 2013

Irani: Je, Dola Inamwogopa Msichana wa Miaka 13?

  30 Aprili 2013

Kuwapiga watu marufuku kusafiri nje ya nchi yamekuwa mazoea ya serikali ya Irani  kwa makusudi ya kuwaghasi wanaharakati wa asasi za kisiasa na zile za kiraia kwa miaka mingi. Lakini, mahakama ya usalama iliwasha moto upya kwa kumpiga marufuku kusafiri nje ya nchi mume wa mwanasheria wa haki za binadamu aliyefungwa Nasrin Sotoudeh pamoja na binti yao mwenye umri wa miaka kumi na mitatu, Mehraveh Khandan. Nasrin Stoudeh amehukumiwa miaka kumi na moja gerezani.

Iran: Wakati Matetemeko yanaua, “Televisheni Zinafundisha Sala”

  21 Aprili 2013

Matetemeko makubwa mawili ya ardhi yalilitikisa eneo la kaskazini magharibi nchini Iran, Mashariki jimbo la Azarbaijan mnamo Jumamosi (Agosti 11, 2012), na kuua watu 250 na kujeruhi karibu 1800. Matetemeko ya ardhi kipimo cha 6.4 na 6.3 katika ukubwa, na kusababisha uharibifu mkubwa na mateso. Wa-Irani waliingia kwenye mtandao wa intaneti ili kuwaombolezea wahanga na kuomba watu kujitolea damu na msaada. Pia walionyesha hasira zao kwa televisheni ya kitaifa ya Iran, ambayo hutangaza vipindi vya dini, badala ya kutoa taarifa kwa watazamaji kuhusu matetemeko ya ardhi na jinsi ya kusaidia.

Misri: Mubarak ahukumiwa kifungo cha maisha

  18 Aprili 2013

Dunia ilishuhudia wakati mahakama ya Misri  ilipomhukumu aliyekuwa Rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak na Waziri wake wa Mambo ya Ndani Habib Al Adly kifungo cha maisha hivi leo kufuatia kukutwa na hatia ya kuhusika na mauaji ya waandamanaji.  Hukumu hiyo ilifikiwa baada ya vikao 49,  masaa 250, na kuandikwa katika kurasa 60,000.

Uturuki: Polisi Watumia Mabomu ya Machozi Kuwatawanya AkinaMama Waandamanaji

  16 Aprili 2013

Wafungwa wa kisiasa wa Kikurdi wamefikia siku yao ya 55 ya mgomo wa kula. Kuna mamia ya wafungwa wa kisiasa walio kwenye mgomo wa kula nchini Uturuki, na hii imesababisha maandamano mshikamano katika bara la Ulaya, na hususani ndani ya Uturuki. Mapema jana [4 Novemba 2012], wanawake ambao ni mama wa baadhi ya wafungwa wa kisiasa walifanya maandamano ya kukaa, na walijikuta wakipambana na mabomu ya machozi, pamoja na kunyunyuziwa maji ya kuwasha. Wa- Kurdi duniani kote wanapinga kimya kinachotumika kushughulikia adha yao.

Syria: Kutwiti Kutokea Vitani Jijini Aleppo

  13 Aprili 2013

Mwandishi wa Habari Jenan Moussa amerudi mjini Aleppo, nchini Syria, akitwiti tajiriba yake wakati vita kati ya vikosi vinavyopinga serikali na vile vinavyoiunga mkono serikali inavyozidi kushika kasi. Twiti za Moussa ni za kawaida na za kibinafsi sana, zikiwapa wasomaji wake taswira ya maisha yalivyo kwa wale walio kwenye uwanja wa vita.

Bahrain: ‘Kususia michezo ya Olimpiki’

  11 Aprili 2013

Wa-Bahraini wengi wanatoa mwito wa kususuia michezo ya Olympics. Kwanza, mwana wa mfalme, ambaye amekuwa akituhumiwa kwa kujihusisha na utesaji wa wanariadha, anahudhuria michezo hiyo. Pili, sehemu kubwa ya timu ya nchi hiyo imetengenezwa na wanariadha wa ki-Afrika.