· Oktoba, 2012

Habari kuhusu Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini kutoka Oktoba, 2012

Misri: Ushauri kwa Waandamanaji wa Kuwait

  27 Oktoba 2012

Wakati watu wa Kuwait walipoanzisha maandamano makubwa ambayo hayakuwahi kutokea ya kuonesha waziwazi kutokukubaliana na mabadiliko ya sheria ya uchaguzi yaliyopitishwa chini ya mtawala wa kurithi kufuatia kuvunjwa kwa bunge, watu wa Misri wametumia muda wao mwingi katika Twita wakitoa ushauri kwa watu wa Kuwait kuhusiana na yapi ya kufanya na yapi ya kutokufanya.

Kuwait: Ni Maandamano Makubwa Kabisa Kuwahi Kutokea?

  27 Oktoba 2012

Mabomu ya kutoa machozi na maguruneti ya kumfanya mtu kupoteza fahamu yalitumika kutawanya maandamano ya kupinga mabadiliko ya sheria ya uchaguzi nchini Kuwait. Maandamano hayo yaliyofanyika siku ya Jumapili, na kuratibiwa kupitia katika mtandao wa Twita na yaliyowavutia takribani watu 150,000 kati ya watu milioni 3 ambao ndio idadi ya watu wa Kuwait. Taarifa za vyombo vya habari zinaichukulia idadi hii kuwa ni kubwa kabisa katika historia ya Falme za ghuba ndogo.

Tunisia: Mgomo Waanza jijini Thala

  8 Oktoba 2012

Kupitia mtandao wa twita, Tounsia Hourra (m-Tunisia huru) anasema [ar] kuna mgomo mkubwa umeanza jijini Thala, kwenye jimbo la Kasserine, leo [Oktoba 8, 2012]. Mgomo huo umekuja kama hatua ya kupinga kukua kwa kasi kwa ukosefu wa ajira na kuzorota kwa maendeleo ya jiji hilo. @tounisiahourra: اضراب عام في تالة...

Uarabuni: Sera ya Romney kwa Mashariki ya Kati Yaibua Mjadala

  8 Oktoba 2012

Hotuba ya Mgombea urais wa Marekani kupitia chama cha Republican Bw. Mitt Romney iliyoelezea sera yake ya nje imeibua mjadala mzito miongoni mwa raia wa mtandaoni leo hasa wale watokao katika nchi za ki-Arabuni. Twiti zinazohoji sera ya mambo ya nje ya Marekani kwa Mashariki ya Kati ziliendelea wakati ambao Romney, anayepeperusha bendera ya chama cha Republican, alipozungumza katika Chuo cha Jeshi cha Virginia. Endapo atachaguliwa, Romney ameahidi kuwa na sera rafiki za mambo ya nje, tofauti na mwelekeo usiotabirika wa sera za Obama wakati huu ambapo mabadiliko ya kisiasa yanaendelea kulikumba eneo la Mashariki ya Kati.