· Septemba, 2010

Habari kuhusu Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini kutoka Septemba, 2010

Irani: Huenda Mwanablogu Aliyefungwa, Hossein Derakhshan (”Hoder”), Akakabiliwa na Hukumu ya Kifo

  25 Septemba 2010

Mwendesha mashtaka huko Tehrani anataka mwanablogu wa Irani aliye gerezani Hossein Derakhshan ("Hoder") apewe adhabu ya kifo. Hakimu bado hajatoa uamuzi. Derakhshan anashtakiwa kwa kosa la “kushirikiana na dola adui, kutangeneza propaganda dhidi ya utawala wa Kiislamu, kutusi utukufu wa dini, na kutengeneza propaganda kwa ajili ya matumizi ya vikundi vinavyopinga mapinduzi." Alitiwa nguvuni miezi 22 iliyopita.

Bahraini: Ali Abdulemam, mwanablogu na mchangiaji wa Global Voices akamatwa

GV Utetezi  6 Septemba 2010

Ali Abdulemam, mwanablogu maarufu wa nchini Bahraini na mwandishi wa Kitengo cha Utetezi cha Global Voices, amekamatwa mapema leo na mamlaka ya nchi ya Bahraini kwa kile anachotuhumiwa nacho kwamba anasambaza “habari za uongo” kupitia mtandao wa BahrainOnline.org, ambao ni moja ya mitandao maarufu zaidi nchini humo inayopigania kuwepo kwa...