· Oktoba, 2009

Habari kuhusu Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini kutoka Oktoba, 2009

Palestina: IDF Yachoma Moto Magari Ya Wapalestina

  28 Oktoba 2009

Kwenye Do Unto Others, Samuel Nichols anaandika kuwa doria ya jeshi la Israel imeanza kuchoma moto magari ambayo yanakamatwa yakijaribu kuvuka mpaka kutoka Ukanda wa Magharibikuingia Israel. Ametundika video hapa.

Uchaguzi Tunisia: haki Bila Ya Upendeleo!!?

  27 Oktoba 2009

Rais wa Tunisia Zine Al Abidine Ben Ali ameshinda uchaguzi kwa kipindi cha tano kwa asilimia 89.62 ya kura zote. Chama chake cha Democratic Constitutional Rally kilishinda viti vya bunge 161 katika viti 214. Wanablogu wa Tunisia wanatoa maoni katika makala hii.

Misri: Watawala Wa Kiimla na Wake Zao

  26 Oktoba 2009

Baada ya kuziangalia picha za mke wa Rais wa Cameroon, Mmisri Zeinobia anasema: “Sijui ni ni kiasi gani cha pesa alichotumia kwa ajili ya nywele zake na muonekano wake lakini ninafahamu kuwa watu wa Camerron wanazihitaji zaidi hizo pesa.”

Uanaharakati na Umama Barani Asia

  24 Oktoba 2009

Je, mwanamke anatoa sadaka zipi ili kupigania jambo analiamini? Je, watoto wake wanaathiriwa vipi na mateso yanayoelekezwa kwake? Makala hii inachambua kwa kifupi maisha ya wanawake wanaharakati katika Asia ambao pia ni ma-mama.

  4 Oktoba 2009

Kutoka Bahrain, Redbelt, anatabiri mwisho wa kublogu.. kama tunavyojua.