Habari kuhusu Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini kutoka Mei, 2009
Tajiri Wa Kimisri Ahukumiwa Kifo
Wamisri walishuhudia hukumu isiyotarajiwa katika historia ya vyombo vya sheria nchini humo: Bilionea Hesham Talaat Moustafa, pamoja na mamluki wake (mpiga risasi wa kukodi) Mohsen El Sokari wamehukumiwa adhabu ya kifo kutokana na kuhusika kwao katika mauaji ya mwimbaji wa Kilebanoni Suzanne Tameem. Mauaji hayo ya kinyama yalitokea huko Dubai, UAE, na hukumu iliyotolewa Alhamisi imesababisha mshtuko na mshangao wakati wanablogu walipojaribu kukubaliana na yaliyotukia.
Saudi Arabia: Je, mafua ya nguruwe yatatishia Hija?
Kila mwaka mamilioni ya Waislamu hukusanyikia Maka kuhiji, moja ya nguzo tano za Uislamu. Je, msimu wa hija ya mwaka huu utatishiwa na homa ya mafua ya nguruwe? Wanablogu wanayo maoni ya kusema.