GlobalVoices katika

Brazil

Kumbukumbu za nchi · 8 jumbe


Habari mpya Kuhusu Brazil

30 Agosti 2012

Brazil: Mtoto wa Miaka 13 Aonyesha Matatizo ya Shule Kupitia Facebook

Diário de Classe [pt], ukurasa wa Facebook uliofunguliwa na Isadora Faber, aliye na miaka 13 na anayetokea Santa Catarina, Brazil, tayari umeonyesha kupendwa zaidi ya mara 176,000. Huku lengo lake likiwa ni “kuonyesha ukweli kuhusu shule za umma”, Isadora anaweka picha zinazoonyesha maeneo yanayohitaji kufanyiwa ukarabati katika shule yake pamoja na kutoa taarifa kuhusu matatizo mengine mengi ya jumla.

31 Julai 2012

Togo: Muhubiri Asafirisha Kilo 4.2 za Madawa ya Kulevya Yaliyofichwa kwenye Pipi ‘k Build Church

Muhubiri wa Injili raia wa Togo, Woegna Yao Koufoualesse alikamatwa katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Accra akiwa na kiasi cha kilo 4.2 za madawa ya kulevya aina ya Cocaine akiwa kwenye safarini kutokea Sao Paulo, chapisho la Afrique Infos linaripoti [fr]. Madawa hayo yalikuwa yamefichwa ndani ya peremende za kijiti; Koufoualesse alijitetea kwamba hakujua kuhusu madawa hayo na kwamba piremende hizo zilikuwa ziuzwe kwa ajili ya kusaidia kupata fedha za kujengea kanisa.

12 Juni 2012

Video jumbe
Brazili: Jarida Lawapa Nafasi Wasio na Makazi

Soma makala hii.

Jarida la Ocas linalosambazwa katika mitaa ya mjini São Paulo pamoja na Rio de Janeiro tangu 2002, ni jarida ambalo husheheni habari ambazo hulitofautisha na vyombo vikuu vya habari nchini Brazil. Na linakwenda zaidi ya hapo. Aidha huwapa mwanzo mpya na fursa za kazi watu ambao hawana makazi na ambao wamo katika hatari ya kuangamia kijamii.

24 Novemba 2009

Video jumbe
Brazil: Je, Milango ya Benki Hubaini vyuma au Rangi za Watu?

Soma makala hii.

Benki nyingi nchini Brazil zinatumia milango inayozunguka yenye vifaa vya kubaini vyuma. Je, milango hiyo inatumika kama kisingizio cha kubagua watu? Video ya uandishi wa kiraia inaonyesha moja ya matukio hayo.

23 Novemba 2009

Photos jumbe
Brazil: Mtazamo wa Wakazi wa Vitongoji Maskini

Soma makala hii.

Katika makala hii, tunasikia mitazamo ya wanahabari raia kutoka mradi wa Viva Favela kuhusiana ya vurugu inayotokana na mihadarati huko Rio de Janeiro na jinsi inavyofagia makazi ya walalahoi, kama wanavyoiona mbele ya milango ya nyumba zao.

6 Novemba 2009

Amerika ya Kati: Kasi Kubwa ya Ueneaji wa Jangwa

Soma makala hii. Conversations for a Better World

Ueneaji wa jangwa unasambaa kimyakimya lakini kwa kasi kubwa mahali pengi duniani na Amerika ya Kati haijaweza kukwepa hali hii iliyo na athari mbaya za kutisha. Wakati ambapo majangwa ni maumbo ya asili, ueneaji wa jangwa ni mchakato wa kuharibika kwa nyanda za ardhi kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na uharibifu unaofanywa na binadamu.

5 Novemba 2009

Video jumbe
Ujauzito na Magereza: Afya na Haki za Wanawake Magerezani

Soma makala hii. Conversations for a Better World

Mapambano bado yanaendelea kuhakikisha haki za binadamu kwa wanawake wajawazito duniani pote, ni inaelekea kwamba katika mchakato huo, wanawake waliopo magerezani wanasahauliwa. Je ni hatua zipi zilizochukuliwa kuhakikisha kuwa nao wanaangaliwa kwa utu, kwa kuzingatia uhai wanaoubeba.

31 Agosti 2008

Photos jumbe
Angola, Brazil: Mshituko na Utengano wa Kitamaduni

Soma makala hii.

Mahusiano maalum kati ya Angola na Brazili yanamaanisha kwamba biashara kati ya makoloni haya mawili ya zamani ya Ureno inashamiri - kadhalika uhamiaji kutoka pande zote za Atlantiki. Lakini, ni vipi hawa watoto wawili wanavyoishi? Ujumbe huu unatoa mitazamo ya wote, kutoka kwa bloga wa Kiangola na wa Kibrazili waishio Luanda.

Sehemu za Dunia

Nchi

Lugha