· Mei, 2014

Habari kuhusu Amerika Kusini kutoka Mei, 2014

Simulizi za Jinsia na Wajibu

  25 Mei 2014

Kwenye blogu ya EnGenerada kuna tafakari ya kina [es] juu ya ujenzi wa utambulisho wa jinsia na masimulizi yanazyohusishwa na wanawake na wanaume. Wanahitimisha kwamba, licha ya kuwa ndugu katika hali halisi, wanafanya kazi kama utaratibu wa kawaida wa kijamii. Makala iliyopitiwa upya hapa ni sehemu ya pili ya #LunesDeBlogsGV...

Gharama na Faida ya Kombe la Dunia Nchini Brazil

  24 Mei 2014

Blogu ya Daniel Bustos kutoka Colombia kuhusu uchumi wa Kombe la Dunia nchini Brazil na baada ya kugusia suala lisilo epukika la rushwa, inasema: Hatimaye, Brazil itatumika kama “panya” kwa mataifa ya Amerika ya Kusini ambayo yalikuwa na ndoto kuwa siku moja itaandaa tukio hili kubwa, itatumika kuuliza kama Brazil...

Colombia: Watoto 32 Wafariki Kwenye Mkasa wa Moto

  24 Mei 2014

Vyombo ya habari Colombia vinaripori [es] vifo vya watoto 32 uliosababishwa na moto katika basi, katika kitongoji cha Fundación mjini Magdalena, Kaskazini mwa Colombia. Tukio hilo la kutisha lilitokea Jumapili mchana, Mei 18, 2014. Hata kama ukweli bado unachunguzwa., Kuna uvumi kwamba gari lilikuwa linasafirisha petroli kimagendo. Rais wa Colombia...

Jumuiya ya Kimataifa na Mgogoro wa Ukraine

  24 Mei 2014

guest blogs [es] ya Angie Ramos [es] katika Tintero kuhusu mgogoro wa kisiasa nchini Ukraine na baada ya kuchambua mambo mbalimbali muhimu husika anahitimisha kwa majibu ya Jumuiya ya Kimataifa: Jambo ni, jumuiya ya kimataifa, inayokabiliwa na kesi kama hii, hufanya vitendo watakavyo kwa kuwa inategemea ukubwa wa maslahi yanayoshiriki...

Wanawake na Matumizi ya Mamlaka ya kisiasa

  17 Mei 2014

EnGenerada anauliza [es] wasomaji wake kama wana kile wanahitaji kutumia nguvu ya kisiasa. Kila siku, tunasoma, kusikia, na kusema maneno: “Siasa ni chombo cha mageuzi ya jamii”. Mawazo yetu yanapokomaa, sisi huangalia katika baadhi ya uhakika wa mazingira yetu, hizo dhana za awali ambazo tumeziingiza kwa vizazi. Wakati huo huo...

Maktaba na Utamaduni Huru

  17 Mei 2014

Blogu kutoka Parque Biblioteca Tomás Carrasquilla – La Quintana, huko Medellin, Colombia, inaelezea [es] msaada wake kwa utamaduni huru. Baada ya kueleze namna ya kuleta utamaduni wa uhuru [es], blogu hiyo inaelezea jinsi inavyoweza kufanya kazi inayofanana na maktaba: Maktaba za umma zaweza kujifunza katika uhuru huu wa kubadilishana taratibu...

Colombia: Hatua za Kudhibiti Mashambulizi ya Kemikali

  9 Mei 2014

Ili kuepusha mashambulizi ya kemikali yanayowalenga hasa wanawake katika maeneo mbalimbali ya nchi, serikali ya Colombia itaanza kudhibiti [es] mauzo ya rejareja ya kemikali ya ‘chokaa’ na vitu vya kemikali kama salfa, haidrokloriki, mariati, chokaa, naitriki na sodiamu haidroksaidi, katika hali ya kimiminika na vipande RCN Radio ilitoa taarifa kwenye...

Madai ya Ukiukaji wa Haki za Binadamu Wakati wa Mgomo wa Kilimo Nchini Colombia

  9 Mei 2014

Tovuti ya ‘kongamano la watu’ imeshutumu hadharani [es] uvunjifu wa haki za binadamu unayoendelea katika mgomo wa kilimo [es] nchini Colombia. Wanaripoti madai ya ukiukaji wa haki za binadamu katika mikoa mbalimbali: Catatumbo na Cucuta, San Pablo-Bolívar, Sogamoso – Boyaca, Kaskazini Santander-Hacarí, Yopal-Casanare, Boyaca, Berlin – Santander, Pinchote – Santander...

Venezuela: Utata na Mashambulizi Wajadiliwa kwenye Mtandao wa Twita

  7 Mei 2014

Wakitumia alama ashiria #UcabCaracas na #SOSColectivosDelTerrorAtacanUCAB [SOS vikundi vya kigaidi vya mashambulizi UCAB], maoni na picha ya mashambulizi kwa wanafunzi kwenye maandamano ambayo inaonekana yalitokea katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Andrés Bello [es] mjini Caracas zimeonyeshwa sana. Miongoni mwa wale wanao twiti ndani ya chuo kikuu hicho, kilchosimamisha shughuli...