Diário de Classe [pt], ukurasa wa Facebook uliofunguliwa na Isadora Faber, aliye na miaka 13 na anayetokea Santa Catarina, Brazil, tayari umeonyesha kupendwa zaidi ya mara 176,000. Huku lengo lake likiwa ni “kuonyesha ukweli kuhusu shule za umma”, Isadora anaweka picha zinazoonyesha maeneo yanayohitaji kufanyiwa ukarabati katika shule yake pamoja na kutoa taarifa kuhusu matatizo mengine mengi ya jumla.
Habari Maalum Kuhusu Latin America
Costa Rica Yakumbwa na Tetemeko la Ardhi wa Ukubwa wa 7.6

Wananchi wa Costa Rica wamekuwa wakitwiti kuhusiana na tetemeko la ardhi lililoikumba nchi hiyo tarehe 5 Septemba saa 2:42 asubuhi, kwa kutumia alama habari #temblorcr and #terremotocr kuhabarishana yanayoendelea.
Pasipoti za Kidiplomasia kwa Viongozi wa Kidini nchini Brazil?

Wizara ya Mahusiano ya Kimataifa ilitoa pasipoti za kidiplomasia kwa viongozi wa kanisa la kiinjili liitwalo World Church of the Power of God, hatua ambayo imewasha majadiliano makali kuhusu dhana ya nchi kutokuwa na dini kama inavyotamkwa katika katiba ya Brazili.
-
Chile: Mahabusu wa Mapuche Wamaliza Mgomo wa Kutokula Uliodumu kwa Siku 60
29 Novemba 2012
-
Venezuela: Tathmini za Baada ya Uchaguzi
15 Oktoba 2012
-
Guatemala: Waandamanaji Wazawa 7 Wauawa Totonicapán
13 Oktoba 2012
-
Venezuela: Ni Chávez Tena kwa Miaka Sita Zaidi
11 Oktoba 2012
-
Venezuela: ‘Sura na Sauti’ za Uchaguzi
8 Oktoba 2012
Habari mpya Kuhusu Latin America
13 Aprili 2013
AZISE ya Uwazi Yajiandaa kwa Uchaguzi wa Jumapili Nchini Venezuela

Wakati wapiga kura wa Venezuela wakijiandaa kuelekea kwenye uchaguzi wa mara ya pili katika kipindi cha miezi sita, kikundi cha Asasi Zisizo za Kiserikali kimekusanya nguvu ili kuhakikisha kuwa wanakuza uwazi katika mchakato wa uchaguzi.
8 Oktoba 2012
Venezuela: Picha za Siku ya Uchaguzi
Leo, mitandao ya kijamii nchini Venezuela inatoa taswira ya nchi hiyo kuwa ukingoni mwa zoezi muhimu. Pamoja na shuhuda mbalimbali, taarifa, tetesi na mapendekezo, majukwaa ya vyombo vya habari vya kijamii kama vile Twita, Facebook na Flickr yameonyesha picha zinazoonyesha ushiriki mkubwa wa watu katika kumchagua Rais ajaye wa Jamuhuri hiyo.
30 Septemba 2012
Mexico: Uandishi Kutoka Gerezani
Enrique Aranda Ochoa writes literature from jail. Convicted of kidnapping in 1997 with a sentence of 50 years in prison, Enrique has used his time in jail to write six novels and earn various literature awards. His latest book, available for purchase in an electronic format, focuses on the mysteries of the Mayans.
28 Agosti 2012

Serikali ya Kolumbia Yapanga Kufanya Mazungumzo na Waasi wa FARC
Katika blogu ya Crónicas, Santos García Zapata anaeleza muktadha [es] kuhusu uamuzi wa Rais wa kuanzisha mazungumzo ya amani na makundi ya waasi. Kongresi ya ‘Kamisheni ya Amani’ imetangaza kwamba Rais Santos “hayupo peke yake” katika dhamira yake ya kupatikana kwa amani.
31 Julai 2012

Togo: Muhubiri Asafirisha Kilo 4.2 za Madawa ya Kulevya Yaliyofichwa kwenye Pipi ‘k Build Church
Muhubiri wa Injili raia wa Togo, Woegna Yao Koufoualesse alikamatwa katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Accra akiwa na kiasi cha kilo 4.2 za madawa ya kulevya aina ya Cocaine akiwa kwenye safarini kutokea Sao Paulo, chapisho la Afrique Infos linaripoti [fr]. Madawa hayo yalikuwa yamefichwa ndani ya peremende za kijiti; Koufoualesse alijitetea kwamba hakujua kuhusu madawa hayo na kwamba piremende hizo zilikuwa ziuzwe kwa ajili ya kusaidia kupata fedha za kujengea kanisa.
21 Julai 2012
Paraguai: Kutoka Kutumikishwa Hadi Kuwa Kiongozi Mzawa.

Kutana na Margarita Mbywangi, ambaye katika umri wa miaka mitano, alichukuliwa kutoka kwa wazazi wake na kuuzwa mara kadhaa na kulazimishwa kufanya kazi za nyumbani. Tangu wakati huo amekuwa kiongozi muhimu wa kabila la Aché na hata kuwa Waziri katika nchi yake. Mbywangi sasa anasimulia maisha yake binafsi kupitia Mradi wa Rising Voices.
12 Julai 2012
Wananchi wa Mexico Wanamchagua Rais Mpya
Mnamo tarehe 1 Julai, Wa-Mexico walipiga kura kumchagua rais wao mpya. Punde tu kura zilipoanza kupigwa, watumiaji wa mtandao wa intaneti walianza kutoa mawazo na uzoefu wao. Walipanga pia namna tovuti na alama ishara za mtandao wa twita zitakavyotumika kukusanya taarifa juu ya udanganyifu na nyendo zilizo kinyume cha sheria wakati wa uchaguzi huo.
7 Julai 2012
Cuba: Maandamano yafanyika Mara Mbili, Wengi Wakamatwa
Kikundi cha wanawake kijiitacho ‘wanawake wavaliao mavazi meupe’ (Ladies in White) kwa mara nyingine wametawala fikra za wanablogu wa Cuba waishio nje ya nchi. Maandamano ya amani ya kikundi hicho ambacho ni moja wapo ya vyombo vya upinzani vinavyoheshimika zaidi katika visiwa hivyo –pamoja na kukamatwa kwao mara kwa mara na vyombo vya dola –yanaendelea kuvuta hisia za watu. Mapambano ya hivi karibuni yalitokea mwishoni mwa juma lililopita wakati wanachama wa kikundi hicho walipojaribu kufanya maandamano mara mbili mjini Havana.
12 Juni 2012
Brazili: Jarida Lawapa Nafasi Wasio na Makazi
Jarida la Ocas linalosambazwa katika mitaa ya mjini São Paulo pamoja na Rio de Janeiro tangu 2002, ni jarida ambalo husheheni habari ambazo hulitofautisha na vyombo vikuu vya habari nchini Brazil. Na linakwenda zaidi ya hapo. Aidha huwapa mwanzo mpya na fursa za kazi watu ambao hawana makazi na ambao wamo katika hatari ya kuangamia kijamii.




























Kiungo cha RSS kwa Latin America 












mambo vipi wanablog muko powa wote.kama mumenisoma nijibuni.
Asante. Nimepita hapa natafuta japan na china wamemalizaje ugomvi wao kuhusu visiwa,pia chanzo cha ugomvi...