· Disemba, 2013

Habari kuhusu Asia Mashariki kutoka Disemba, 2013

China: Mashindano ya “Akina Mama Wanaotamanisha”

  23 Disemba 2013

Sina Weibo, tovuti ya Kichina inayofanana na Twitta, imeandaa mashindano ya “Akina Mama Wanaotamanisha.” Picha za washindani zinaonyesha wazi kwamba wengi wao sio akina mama halisi. Hata hivyo, hizo picha zinatuambia mengi kuhusu uhusiano wa kijinsia nchini China. Soma mengine kwenye tovuti ya Offbeat China.

Mandela na Mao, Hawakushabihiana sana.

Jeremiah kutoka katika studio ya Granite atoa maoni yake kwenye Televisheni ya Taifa ya China, CCTV akitaka kuonesha uhusiano uliokuwepo kati ya Mandela na Mao Zedong: Mandela hakushabihiana sana na Mao. Mao alikuwa muumini wa udhanifu kama tafsiri ya neno linavyotanabaisha, mtu aliyeamini kuwa, mchakato wa utendaji wa jambo ndilo...

Kimbunga Haiyan: Hadithi ya Ujasiri Kupitia Filamu Fupi

  17 Disemba 2013

Kimbunga Haiyan, filamu fupi kwa hisani ya Janssen Powers, inaonyesha hali baada ya dhoruba ambayo mapema mwezi Novemba iliua zaidi ya watu 6,000 katika jimbo la Philippine la Leyte. “Kwa kawaida, mimi nia yangu ilikuwa kupata habari za uharibifu huo, “Powers aliandika katika maelezo ya kazi yake. “Nilicho pata hata...

Sababu za Ajali Barabarani Mjini Bangkok

  10 Disemba 2013

Cha kushangaza, polisi mjini Bangkok, Thailand wanadai kwamba asilimia 30 ya ajali za barabarani husababishwa na ‘magari yasiyostahili kuwa barabarani’ wakati yanayo endeshwa kasi ni asilimia 5 ya ajali. Mwandishi Thitipol Panyalimpanun anabainisha kuwa katika nchi nyingi, ajali za barabarani hulaumiwa kwa makosa dereva na si juu ya magari.

Taiwan: Maandamano Dhidi ya Sheria Juu ya Usawa Kwenye Ndoa

  3 Disemba 2013

Wabunge wa Yuan nchini Taiwan walipitisha muswada wa kwanza ya “Usawa kwenye Ndoa“ [zh] mnamo Oktoba 25, 2013. Novemba 30, zaidi ya watu 300,000 walipinga muswada huu, hasa dhidi ya pendekezo juu ya ndoa za jinsia moja. J. Michael Cole, mwandishi wa habari wa kujitegemea mkaazi wa Taipei, alielezea kile...

China: Jukumu la Baba

  2 Disemba 2013

Mtandao wa Offbeat China umeanzisha kipindi kipya na maarufu cha televisheni kinachojulikana kwa jina la “Baba, tunaelekea wapi?”. Kipindi hicho kinawakutanisha akina baba watano maarufu pamoja na watoto wao kwa ajili ya kufanya kazi mbalimbali za nje kwa lengo la kushindana na bila ya uwepo wa wake zao. Hapa chini,...