The Global Voices Lingua project hopes to bring GV content to new linguistic audiences - Details

Also in:

East Asia Kumbukumbu za sehemu

Kiungo cha RSS kwa East Asia

2009-11-17

China ,
U.S.A.

Adam Minter amesikitishwa na maoni ya Obama kwenye Mkutano uliofanyika kwenye Ukumbi wa Jiji la Shanghai, hasa, maelezo yake kuwa “Mimi ni muunga mkono mkubwa wa kutokuchuja habari“.

2009-11-14

Philippines: Mti wa Dita Waokoa Maisha ya Watu 36 Wakati wa Mafuriko

Mti wa aina ya Dita huko Manila mjini uligeuka kuwa "Mti wa Uzima" wakati ulipotumika kama kimbilio na wakazi ambao walitegwa kwenye nyumba zao wakati wa janga la kimbunga na mafuriko ya hivi karibuni. Somo: Usikate miti.

2009-11-06

Tamasha la Blogu IndonesiaPhotos postVideo post

Tulitembelea tamasha la blogu la Indonesia au PestaBlogger 2009. Hii nim ara ya tatu kwa tukio hili la mwaka kufanyika. Tukio hili lilishuhudia wanablogu kutoka kila sehemu ya Kisiwa hiki ambacho pia ni Taifa wakimiminika mjini Jakarta ili kusherehekea, kujadili na kujumuika.

Vietnam

Charvey amebaini matangazo mengi kuliko kawaida katika uwanja wa ndege wa Vietnam.

2009-11-02

Japan: Mkeo anapougua

Pale utamaduni wa "mifugo ya mashirika" au kwa maneno mengine “utamaduni wa ujumla wa wafanyakazi” (社蓄 shachiku) na maadili ya ndoa vinapogongana - zaidi ya watu 300 walitoa majibu kuhusiana na swali lililoulizwa kwenye jukwaa kubwa la mijadala lijulikanalo kama Hatsugen Komachi: Je, mwanaume aombe ruhusa kazini pale mkewe anapougua? Hali ...

2009-10-27

Malayasia: Serikali ya Jimbo Yaja na Sera ya ‘Msala Mmoja’

Kwa kuiga chapa ya Malaysia1, serikali ya Jimbo la Terengganu hivi majuzi ilikuja na sera ya ‘msala 1’ kama hatua kwa walimu na wanafunzi (wa jinsia moja) kuchangia misala (vyoo) ili kukuza hisia za umoja. Kumekuwepo na maoni mchanganyiko katika ulimwengu wa blogu kuhusiana na sera hii.

2009-10-26

Cambodia: Tuzo yamuenzi aliyenusurika na utumwa wa ngonoVideo post

Sina Vann alikuwa na umri wa miaka 13 wakati alikupoja Cambodia kutoka Vietnam kwa kile kilichopaswa kuwa likizo. Badala yake, aliuzwa kama mtumwa kwa ajili ya ngono na alitumia miaka miwili iliyofuata ndani ya danguro. Alikombolewa wakati Somaly Mam, mwanaharakati wa kupinga utumwa na sura ya Taasisi ya Somaly Mam, ...

Japan: Uchunguzi Mpya Juu ya Umaskini Waharibu Soga za Utajiri

Mjapani mmoja kati ya sita anaishi katika umasikini inasema ripoti mpya ya Wizara ya Ustawi wa Jamii [en]. Kwa mujibu wa takwimu za OECD, Japan ina kiwango kikubwa zaidi cha umasikini katika dunia iliyoendelea na ni ya 4 baada tu ya Mexico, Uturuki na Marekani. Mnamo mwezi wa Septemba, Makoto Yuasa, ...