GlobalVoices katika

Trinidad & Tobago

Kumbukumbu za nchi · 8 jumbe


Habari mpya Kuhusu Trinidad & Tobago

9 Oktoba 2012

Trinidad na Tobago: Ufisadi na Utawala wa Sheria

Hivi karibuni, masuala ya utawala wa sheria yamekuwa yamekuwa yakitawala serikali iliyoko madarakani. Kwa kuwa na kipengere cha 34 ambacho hakifahamiki sana miongoni mwa wananchi, hali ya mambo imebadilika na kuwa utawala wa kiimla, na [...] tunaweza kuona ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka yamebadilisha kabisa tabia za wale tuliowaona kama nguzo na mifano ya kuigwa katika jamii yetu.

Jumbie's Watch anaandika kuhusu utawala na kuheshimiwa kwa sheria katika nchi ya Trinidad & Tobago.

31 Disemba 2011

Video jumbe
Dondoo za Video: Maandamano, Chaguzi, Utamaduni na GV

Soma makala hii.

Baadhi ya habari za kuvutia za Global Voices na video za hivi karibuni kutoka Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara, Mashariki na Ulaya Kati, Karibeani pamoja na Marekani ya Kusini, zimeletwa na Juliana Rincón Parra.

15 Disemba 2009

Barbados, Trinidad & Tobago:Plastiki na Uchafuzi wa Mazingira

“Fanya matembezi kwenye pwani yoyote nchini Barbados – na utaona uchafu wa plastiki uliosukumwa ufukweni”: Barbados Free Press anauliza kama uuzaji wa chupa za plastiki za maji uwekewe vikwazo, wakati Mtrinidadi Keith Francis pia anaguswa na suala la uchafuzi wa mazingira kwa plastiki ulimwenguni.

28 Oktoba 2009

Caribbean: Tafakari Mpya Kuhusu Uchapishaji wa Mtandaoni

Soma makala hii.

Wanablogu wa ukanda wa Karibea wanawaza kuanzisha jumuiya ya uandishi na uchapishaji ya mtandaoni ikitumia njia za mawasiliano zilizo shirikishi ili kukabiliana na ugumu wa uchapishaji vitabu unaoukabili ukanda wao.

26 Oktoba 2009

Trinidad & Tobago: Kampeni ya 350

“Trinidad na Tobago ni kisiwa tajiri na nchi inayoendelea tajiri kwa mafuta na gesi asilia. Lakini pia tunashuhudia madhara mabaya ya maendeleo ya haraka kwenye nyanja za viwanda katika visiwa vyetu. Hii ni fursa ya sauti za wanawake kusikika”: Attillah Springer anajihusisha na kampeni ya hali ya hewa 350.

24 Oktoba 2009

Trinidad & Tobago: Mtrini Mpaka Kwenye Mifupa?

“Kila siku ambayo ninapitia habari ninazidi kushawishika kuwa ninataka kuachana na klabu ya ‘Mimi ni Mtrini’ na kwenda sehemu nyingine”: Coffeewallah ameshachoka na kila kitu kuanzia uhalifu mpaka kodi.

17 Februari 2009

Jamaika: Miziki Yenye Maneno Machafu Yazuiwa

Soma makala hii.

Utata wa muda mrefu juu ya usahihi wa kurushwa hewani kwa miziki fulani umezuka tena nchini Jamaika. Wanablogu wa Jamaika wanapaza sauti zao.

20 Agosti 2008

Karibeani: Radi ya Bolt Yaipiga Beijing

“Radi ya Bolt” – Picha na hybridvigour. Tembelea mtiririko wa picha zake. Ujumbe huu utakuwa mrefu kama ufupi wa mtoko wa Mjamaika Usain Bolt kuelekea chaki ya ukomo wa mbio...

Sehemu za Dunia

Nchi

Lugha