2009-02-15
Haiti: Fanmi Lavalas na Uchaguzi Ujao
Mwishoni mwa juma lililopita, ulimwengu wa wanablogu wa Kihaiti ulijaa habari za kutengwa kwa vyama vya siasa na Tume ya Muda ya Uchaguzi kwenye uchaguzi wa maseneta utakaofanyika mwezi Aprili 2009 , na siku ya tarehe 6 Januari, tume hiyo CEP ilichapisha orodha ya wagombea ubunge watakaokwaana kwenye uchaguzi ujao wa bunge nchini Haiti. Wanablogu wanaandika mawazo yao kuhusu wagombea walioachwa.
2009-02-02
Mashariki ya Kati: Vikwazo kama Silaha ya Kisiasa
Watu wengi wa Mashariki ya Kati wamesusia bidhaa za Israeli na Marekani kama jibu la mashambulizi ya Israeli huko Gaza. Tarek Amr anapitia yale wanablogu wanayosema kuhusu suala hili.
2009-01-26
MENA: Maoni Wakati Wa Kuapishwa Obama
Tukio la kihistoria limetokea Marekani leo wakati Barack Obama alipoapishwa kuwa rais wa 44. Wakati kuungwa mkono kwa Obama kati ya Waarabu kumekuwa kukipungua katika miezi michache iliyopita kufuatia uteuzi wake wa baraza la mawaziri na ukimya wake kuhusu mashambulio ya Israeli huko Gaza, wanablogu wa Mashariki ya Kati na ...
2008-11-09
Iraki:OBAMAAAAA!!! Huraaah Oyee!!
Hivyo ndivyo asemavyo Neurotic Iraqi Wife. Kwa ujumla blogu nyingi za Iraki zimemchukulia vyema rais mteule Obama, lakini sio wanablogu wote waliofurahia. Salam Adil anaorodhesha maoni baada ya Uchaguzi wa rais huko Marekani.
2008-10-28
Chile: Mkutano wa McCain na Pinochet Mwaka 1985
2008-10-26
Bahrain: Raha na Karaha za Kusoma Ng'ambo
Ingawa Bahrain ina idadi kadhaa ya vyuo vikuu, vya umma na binafsi, raia wengi wa nchi hiyo hupata fursa ya kwenda ng'ambo kwa masomo ya shahada ya kwanza na hata zile za juu, mara nyingi kwa kutegemea ufadhili. Moja ya matatizo ya kwanza wanayokumbana nayo huko ughaibuni ni kwamba watu wachache tu hufahamu ni wapi Bahrain ilipo. Katika makala hii tunafuatilia uzoefu wa wanablogu watatu ambao ndiyo kwanza wamekwenda ng'ambo kwa masomo: kule Japan, Uingereza na Marekani na mwanablogu wa nne ambaye anasoma India kwa kipindi fulani hivi sasa.
2008-10-15
Macho ya Kimataifa kwenye Uchaguzi wa Marekani
Kadiri uchaguzi wa Marekani unavyokaribia, ndivyo kadiri macho ya kimataifa yanavyozidi kuelekezwa katika sera za nje za taifa hilo na wagombea wake wakuu. Kazimiradi kama vile ile ya Collective Journalism inayofanywa na Current TV (Uandishi wa Habari wa Umma wa Current TV) na Global Voices' Voices Without Votes (Mradi wa Global Voices - Sauti Zisizo na Kura) zimechukua jukumu la kukusanya taarifa na kuzipa mtazamo wa kimataifa katika masuala ya ndani ya sehemu fulani tu ulimwenguni.



