The Global Voices Lingua project hopes to bring GV content to new linguistic audiences - Details

Also in:

Americas Kumbukumbu za sehemu

Kiungo cha RSS kwa Americas

2009-12-02

Video: Vijana duniani kote wajieleza kwa sekunde 60Video post

mradi wa OneMinuteJr unawapa vijana......

2009-11-23

Brazil: Mtazamo wa Wakazi wa Vitongoji MaskiniPhotos post

Katika makala hii, tunasikia mitazamo ya wanahabari raia kutoka mradi wa Viva Favela kuhusiana ya vurugu inayotokana na mihadarati huko Rio de Janeiro na jinsi inavyofagia makazi ya walalahoi, kama wanavyoiona mbele ya milango ya nyumba zao.

2009-11-17

China ,
U.S.A.

Adam Minter amesikitishwa na maoni ya Obama kwenye Mkutano uliofanyika kwenye Ukumbi wa Jiji la Shanghai, hasa, maelezo yake kuwa “Mimi ni muunga mkono mkubwa wa kutokuchuja habari“.

Paraguay: Wenyeji Wanyunyiziwa Dawa za Kuua Wadudu kwa Ndege

Huko Mashariki mwa Paraguay, jumla ya watu 217 wa jumuiya ya wenyeji ya Ava Guaraní walianza kusumbuliwa wakionyesha dalili mbalimbali za kiafya zinazoaminika zilisababishwa na unyunyiziaji wa makusudi wa dawa za kuua wadudu hasa baada ya wao kuwa wamegoma kuhama kutoka katika ardhi waliyoirithi kutoka kwa mababu zao.

2009-11-16

Senegal ,
Haiti

Wiki hii, waandishi wawili wenye asili ya Kiafrika wanaoandika kwa Kifaransa walipewa tuzo mbili zenye kuheshimika sana katika fasihi ya Kifaransa: Ulimwengu wa blogu za wanaozungumza Kifaransa katika Karibea umekuwa ukinguruma juu ya kutosheka kwao mara mbili kwa mpigo, katika makala hii kutoka Haiti, na hii kutoka Guadeloupe na hii kutoka Martinique [Fr].

2009-11-14

Marekani: Mauaji ya Fort Hood Yasababisha Kumulikwa kwa Waislamu Walio JeshiniVideo post

Shambulizi la upigaji risasi la kushtukiza lililofanywa na mwanajeshi wa Jeshi la Marekani, Meja Nidal Malik Hassan, na kusababisha vifo vya watu 13 na kujeruhi wengine 31 katika kambi ya kijeshi ya Fort Hood, jimbo la Texas, kwa mara nyingine limesababisha Waislamu nchini Marekani kumulikwa - hasa wale wanolitumikia jeshi.

2009-11-13

Venezuela: Kukutana na kazi za msanii Jesus Soto

Kazi za msanii wa Kivenezuela Marehemu Jesus Soto zinapaswa kuguswa na kujizamisha ndani yake ili kuzielewa. Wachache waliwahi kutembelea kazi zake kwenye makumbusho wameandika uzoefu wao.

2009-11-11

Video: Dunia Yaadhimisha Kuanguka kwa Ukuta wa BerliniVideo post

Leo ni Kumbukumbu ya 20 ya kuanguka kwa Ukuta wa Berlini, kizingiti madhubuti cha kiusalama ambacho kiliwahi kuligawa jiji la Berlini katika pande mbili za Mashariki na Magharibi huko Ujerumani. Leo tunaonyesha baadhi ya picha za video zinazotoka pande mbalimbali za dunia zinazopandishwa ili kusherehekea siku hii na nini ukuta huo ulimaanisha siyo Ujerumani tu bali duniani kote.