· Oktoba, 2012

Habari kuhusu Video kutoka Oktoba, 2012

Kuwait: Ni Maandamano Makubwa Kabisa Kuwahi Kutokea?

Mabomu ya kutoa machozi na maguruneti ya kumfanya mtu kupoteza fahamu yalitumika kutawanya maandamano ya kupinga mabadiliko ya sheria ya uchaguzi nchini Kuwait. Maandamano hayo yaliyofanyika siku ya Jumapili, na kuratibiwa kupitia katika mtandao wa Twita na yaliyowavutia takribani watu 150,000 kati ya watu milioni 3 ambao ndio idadi ya watu wa Kuwait. Taarifa za vyombo vya habari zinaichukulia idadi hii kuwa ni kubwa kabisa katika historia ya Falme za ghuba ndogo.

Zambia: Filamu yaYouTube Kuhusu Athari za Machimbo ya Madini

Filamu ya Uchunguzi yenye jina "Zambia: Shaba Nzuri, Shaba Mbaya" inayohusu machimbo ya shaba nchini Zambia na athari zake kwa jamii imewekwa kwenye mtandao wa YouTube na mpaka sasa imevuta watazamaji zaidi ya 6,000. Baada ya kuitazama filamu hiyo, mtumiaji mmoja wa mtandao wa YouTube aliandika, "Jililie eeh nchi yangu nzuriKwa nini tubaki masikini katikati ya utajiri huu wa madini yanayochimbwa kwa gharama ya afya za wenyeji?"