· Juni, 2012

Habari kuhusu Video kutoka Juni, 2012

Kenya: Kilimo cha Bustani Mijini Chashika Kasi

Nchini Kenya, wakazi wa mjijini wanajifunza mbinu mbalimbali za kulima mazao ya chakula kwa ajili ya matumizi binafzi na kwa ajili ya kuuza katika maeneo madogo. kwa watu wenye kipato kidogo au wasio na kipato, ukulima wa mijini unaweza kuwa ndiyo ufumbuzi wa kujihakikishia uwepo wa chakula. Video hizi zinaonyesha jinsi ambavyo chakula kinaweza kuzalishwa katika makasha na vifaa vingine vya kubebea kwa kutumia maeneo na rasilimali kidogo.

Ethiopia: Ardhi, Historia na Haki katika Eneo la Gambella

Wanaharakati wa masuala ya ardhi wanatumia hati ya malalamiko ya mtandao, mtandao wa facebook na twita kufanya kampeni dhidi ya unyang’anyi wa ardhi nchini Ethiopia. Inaarifiwa kwamba wanakijiji kwenye jimbo msikini zaidi nchini humo, Gambella, wanalazimishwa kuhamia kwenye vijiji vilivyobuniwa na serikali ili kuwapisha wanaoitwa 'wawekezaji' wakubwa.

Brazili: Jarida Lawapa Nafasi Wasio na Makazi

  12 Juni 2012

Jarida la Ocas linalosambazwa katika mitaa ya mjini São Paulo pamoja na Rio de Janeiro tangu 2002, ni jarida ambalo husheheni habari ambazo hulitofautisha na vyombo vikuu vya habari nchini Brazil. Na linakwenda zaidi ya hapo. Aidha huwapa mwanzo mpya na fursa za kazi watu ambao hawana makazi na ambao wamo katika hatari ya kuangamia kijamii.