· Aprili, 2011

Habari kuhusu Video kutoka Aprili, 2011

Naijeria Yapiga Kura 2011: Maoni kutoka kwenye Uchaguzi

Wanaijeria walipiga kura jana katika uchaguzi wa tatu wa rais tangu taifa hilo lilipoingia kwenye utawala wa kiraia mwaka 1999. Mpaka sasa, uchaguzi huo umeelezwa na wengi kuwa ulikuwa wa mafanikio, huku kukiwa na taarifa za ghasia za hapa na pale pamoja na hitilafu za upigaji kura. Vyanzo vya habari vimeripoti kuwa watu wengi walijitokeza, foleni zenye kufuata utaratibu, na wapiga kura kusubiri hadi uchaguzi utakapomalizika ili kuhakikisha kwamba kura zao zimehesabiwa. Wanablogu wanajadili.

Côte d'Ivoire: Kuanguka kwa Laurent Gbagbo

Laurent Gbagbo alikamatwa katika makazi yake ya Cocody, pamoja na mkewe, Simone, na msafara wa watu wa karibu. Miezi mitano baada ya kukataa kukabidhi madaraka kwa rais anayetambuliwa kimataifa kama rais mpya wa Côte d'Ivoire, Alassane Ouattara, mgogoro nchini humo hivi sasa unaelekea kufikia hitimisho.Mtiririko wa matukio yaliyopelekea kukamatwa kwa Gbagbo yaliorodheshwa kwa kina kwa njia ya video za kwenye mtandao ambazo zilitolewa maoni kwenye mtandao.

Côte d'Ivoire: Gbagbo agoma, Waafrika waandamana

Wakati Rais wa zamani wa Côte d'Ivoire Rais Laurent Gbagbo akiwa bado amejichimbia ndani ya handaki nchini humo, akigoma kukamatwa kwa kuendelea kukataa kushindwa kwenye uchaguzi wa mwaka 2010, ushiriki wa Ufaransa katika harakati za kumng’oa zinasababisha miitikio miongoni mwa wanasiasa na raia wa Ufaransa, pamoja na jamii ya Waafrika waishio Ufaransa.