Habari kutoka Muhtasari wa Habari na Pakistan
Pakistan, Usiingilie Vita vya Ndani ya Syria
Siku moja baada ya dondoo ndogo ya habari yenye kichwa cha habari, “Saudi Arabia ‘inatafuta uungwaji mkono kwa waasi wa” ilipoonekana kwenye magazeti ya Pakistani, mwanablogu wa siasa Ahsan Butt aliposti tahadhari kali kwa watunga sera ya mambo ya Kimataifa wa nchi ya Pakstani kuachana na mambo ya ndani ya...
Sababu 10 Kwa nini Siafiki Shariah Nchini Pakistan
Mmoja wa msemaji wa Taliban alijitoa kwenye majadiliano ya hivi karibuni na serikali ya Pakistan na kudai kuwa ajenda ni pamoja na kuanzishwa kwa sharia kali. Mwanablogu wa Pakistan na Mwandishi wa Habari Beena Sarwar alipinga wazo hilo kupitia tamko aliloliweka katika mtandao wa Facebook lenye kichwa cha habari ‘sababu...
Nani ni Muislamu Halisi? -Hatari ya Madhehebu Madogo ya Waislamu Pakistan
Raza Habib Raja wa Pak Tea House ana maoni haya: ‘Kosa’ kubwa nchini Pakistani ni kuwa kile ninachokiita, Muislamu asiye Muislamu. Kwa hiyo hata ukiwa Ahmedi, Shiite, na hata muumini wa Mtakatifu Sufi bado utaitwa Asiye Muislamu na baadhi ya watu. Hilo linatuleta kwenye swali “nani ni Muislamu?” Raja anaeleza:...
Kuwasaidia Waathirika wa Tetemeko la Balochistan
Zaidi ya watu 300,000 wameathirika kufuatia tetemeko la hivi karibuni katika wilaya sita za Jimbo la Balochistan nchini Pakistan. Kashif Aziz wa mtandao wa Chowrangi anatoa habari za namna ya kutoa msaada kwa waathirika wa tetemeko la Balochistan.
Pakistani: ISI Walikuwa Wanafahamu Nini Kuhusu Laden?
Faheem Haider katika blogu ya Sera ya Nchi za Nje ya Pakistani anahoji kile ambacho Jeshi na Usalama wa Taifa (shirika la kijasusi) la Pakistani vilikuwa vinafahamu kuhusu gaidi mkuu Osama Bin Laden, ambaye aliingiliwa na kuuwawa huko Abbottabad, karibu na mji mkuu wa Pakistani.
Pakistani: Katika Vita
Mohammad Malick anatoa maoni juu ya shambulizi la kigaidi la hivi karibuni kwenye soko la watu wa tabaka chini na la kati huko Peshawar: “limeonyesha kuwa hii ni vita ambyo magaidi wanasimama upande mmoja wa mstari wa damu, na sisi wananchi upande mwingine.”