Habari kutoka na

Uhamaji wa Watoto Wachukuliwa kuwa ni Baa la Kibinadamu

  26 Juni 2014

Kutoka Mexico, Katia D'Artigues, ambaye ni mwandishi wa blogu ya Campos Elíseos (Champs Elysées), aandika kuhusiana na watoto kulazimika kuhama wao wenyewe [es], hali inayompelekea kuiita hali hii kuwa ni “baa la kibinadamu”: Son niños que son orillados a cruzar la frontera solos. No lo hacen por aventura, sino porque...

Wahamiaji 87 Wafariki kwa Kukosa Maji Kaskazini mwa Niger

Mnamo tarehe 30 0ctoba, watu 87 waliokuwa wakijaribu kuifikia bahari ya Mediterania walifariki mara baada ya madereva waliokuwa wakiendesha magari waliyoyatumia kusafiria kuwatelekeza wahamiaji hao katika Jangwa la Sahara. Wahamiaji hawa walihangaika kutafuta msaada bila ya mafanikio. Simulizi ya kuhuzunisha kutoka kwa mmoja wa watu walionusurika aliyejulikana kwa jina la...

Lebanoni: Wafanyakazi wa Ndani Wanaotoroka

“Mfanyakazi wa ndani anapotoroka kutoka kwenye nyumba ya mwajiri wake, kituo cha polisi hakiwezi kufanya lolote kwa sababu hakuna sheria dhidi ya wafanyakazi wa ndani wanaotoroka. Kwa hiyo ofisa wa kituo cha polisi anamwambia mwajiri wa ki-Lebanoni aseme kuwa (mtoro huyo) aliiba pesa,” anaandika Ethiopian Suicides.