Habari kutoka Muhtasari wa Habari na Lebanon
Lebanon: Mwanablogu Apata Kipigo kwa Kupiga Picha
Mwanablogu wa ki-Lebanoni Habib Battah anaeleza namna alivyoshikiliwa bila hiari, akilazimishwa kufuta picha katika kamera ya simu yake na kudhalilishwa mfululizo katika posti hii inayohusiana na ripoti ya Beirut. Aliporipoti suala hilo katika kituo cha polisi mahali alipokuwa, mafisa wanaohusika walimkana na kumgeuzia kibao yeye. Anaongeza: Walikuwa sahihi. Kama watu...
Lebanoni: Wafanyakazi wa Ndani Wanaotoroka
“Mfanyakazi wa ndani anapotoroka kutoka kwenye nyumba ya mwajiri wake, kituo cha polisi hakiwezi kufanya lolote kwa sababu hakuna sheria dhidi ya wafanyakazi wa ndani wanaotoroka. Kwa hiyo ofisa wa kituo cha polisi anamwambia mwajiri wa ki-Lebanoni aseme kuwa (mtoro huyo) aliiba pesa,” anaandika Ethiopian Suicides.
Lebanoni: Matukio ya Wafanyakazi Kujiua ‘Yanadharauliwa’
Matthew Cassel anaripoti tukio la kujia la Theresa Seda, mfanyakazi wa ndani wa Kifilipino jijini Beirut. Soma habari za kina za kutisha za jinsi vifo vya namna hiyo vinavyoongezeka kwa idadi – vinaendelea kutotiliwa maanani kwenye Justimage.