Habari kutoka Muhtasari wa Habari na Sheria
Kuhusu Uamuzi wa Mahakama wa Haki ya Kusaidiwa Kufa Nchini Afrika Kusini
Profesa Pierre de Vos anaingia rasmi kwenye mjadala mkali kuhusu uwezekano wa kumsaidia mtu kufa nchini Afrika Kusini baada ya Mahakama Kuu nchini humo kuamua kwamba mtu anayekufa ana haki ya kusaidiwa kufa na daktari ili aweze kuyahitimisha maisha yake: Ni muhimu kuona kwamba hukumu hii haimlazimishi mtu kuyakatisha maisha...
Kulinda Taarifa Binafsi Nchini Ajentina Bado Kuna Safari Ndefu
Kwenye makala iliyoandikwa kwa ajili ya gazeti la mtandaoni Haki za Kidijitali: Amerika Kusini & Visiwa vya Caribbean, No.21, Mmwanasheria wa ki-Ajentina Valeria Milanés anaeleza kwamba hata kama Marekani ni kiranja wa dunia kwenye kuchakata taarifa (data), bado haina sheria ya kulinda taarifa za watu. Marekani pia inachukuliwa kama nchi yenye “kiwango...
Video: Mwanasheria wa Swaziland Aliyefungwa Jela Azungumza Kupitia Wanaharakati wa Haki za Binadamu
#swazijustice ni kampeni inayotoa wito wa kuachiliwa huru kwa Bheki Makhubu, mhariri wa gazeti la Taifa na Thulani Maseko, mwanasheria wa haki za binadamu, ambao walifungwa jela nchini Swaziland kwa miaka miwili kwa sababu ya kuandika makala kukosoa mfumo wa mahakama nchini humo. Wawili hao walikamatwa tarehe 17 Machi 2014...
Kuongozeka kwa Vitendo vya Kujichukulia Sheria Mkononi Nchini Senegali
Sada Tangara, mpiga kura na mwanablogu anayeishi Dakar, nchini Senegali aliweka picha-habari inayohusu kuongezeka kwa matukio ya kujichukulia sheria mkononi kwenye mitaa ya Dakar, mji mkuu wa Senegali. Anaeleza mwanzo wa mradi wake na kwa nini aina hii maarufu ya haki imeshika kasi jijini Dakar [fr] : Il faut savoir...
Udhalilishaji wa Kijinsia wa Watoto Wanaotalii Asia ya Mashariki
Mradi wa Nguzo ya Kuokoa Utoto, uliobuniwa na serikali ya Australia, umezinduautafitiukosefu wa msaada wa kijamii, elimu, furasa na ulinzi” kwa kuendelea kwa vitendo vya kuwadhalilisha watoto. Utafiti huo pia umeonyesha namna kusafiri na utalii “ni hatari nyingine inayochangia shida za kudhalilishwa zinazowakumba watoto.” Utafiti huo ulihusisha nchi za Thailand,...
Maandamano Makubwa Yafanyika huko Guangzhou, China
Mamia ya wakazi wa Guangzhou jana mchana walikusanyika huko Sanyuanli kupinga hatua ya polisi ya kutaifisha mali binafsi za watu kwenye bohari kama sehemu ya harakati za kukabiliana na majanga ya moto. Waandamanaji walijikuta wakikabiliana vikali na polisi, na baadae, wakati wa vurugu hizo, waandamanaji walifikia hatua ya kupindua magari...
Twiti za Moja kwa Moja za Kesi Dhidi ya Mwanasheria wa Haki za Binadamu na Mwandishi wa Habari Nchini Swaziland
MISA-Swaziland anatwiti moja kwa moja mwenendo wa mashitaka dhidi ya mwanasheria wa haki za binadamuThulani Maseko na mwandishi wa habari Bheki Makhubu bila ruhusa ya mahakama nchini Swaziland. Wawili hao walikamatwa mnamo Machi 17, 2014.
Macau: Watu 3,000 Wazunguka Baraza la Wawakilishi Kukwamisha “Muswada wa Walafi”
Taarifa zaidi zinapatikana kwenyetaarifa yetu ya awali ya GV.
Mapigano ya Wanakijiji Kugombea Ardhi Yasababisha Maafa Nchini Madagaska
Blogu ya L'Express Mada ilitoa taarifa kwamba kijiji kizima cha Andranondambo kilichoko Kusini mwa Madagascar kiliharibiwa [fr] kufuatia mapigano ya wanakijiji yaliyosababishwa na mzozo wa kumiliki ardhi. Vita vya wenyewe kwa wenyewe, ambayo ilidumu kwa siku tatu kati ya Mei 20-22, ilipoteza maisha ya wanakijiji wote. Akikumbuka tukio hilo, mmoja...
Jamaika: Alama Zinapoashiria Kikomo
Blogu ya Active Voice imetoa mkusanyiko wa twiti zenye mitazamo ya kupendekeza ufumbuzi kuhusu kampeni ya #bringbackourgirls inayodai kurudishwa kwa wasichana waliotekwa na magaidi wa Boko Haram.