Habari kutoka Muhtasari wa Habari na Uchumi na Biashara
Makampuni ya Teknolojia Nchini Kenya Yaliyofadhiliwa Mwaka 2014
Je, unayajua makampuni ya teknolojia nchini Kenya yaliyopata ufadhili kwa mwaka 2014? Erik Hersmann anayaorodhesha kwenye blogu yake: Fedha za mtaji wa awali Angani – Huduma za mtandao wa umma wa kompyuta BRCK – Huduma za mtandao wa Si-Waya za WiFi CardPlanet – Mfumo wa malipo kwa njia ya simu...
Ufisadi Uliofanywa na Makampuni Makubwa Katika Kupambana na Ebola Nchini Sierra Leone
Makampuni matano nchini Sierra Leone yanasemekana kutumia fedha zilizokusudiwa kupambana na Ebola kwa njia za kifisadi: Haya hapa makampuni matano yaliyokuwa yameingia mikataba mikubwa ya kusambaza vifaa na kutoa huduma katika kupambana na ugonjwa wa Ebola nchini Sierra Leone kama yalivyoorodheshwa kwenye Taarifa ya Ukaguzi ya Fedha za Kupambana na...
Taarifa ya Maendeleo ya Kiteknolojia Barani Afrika
Erik anatushirikisha taarifa 5 kuhusu mwenendo wa teknolojia barani Afrika: Nimeendelea kutamani kuandika makala za blogu kuhusu taarifa hizi moja baada ya nyingine, nyingi zikihusu Afrika, lakini inaonekana sitaweza. Badala yake, nitaweka kiungo cha kila moja wapo, inayoonekana, na maneno machache ya kwa nini ni muhimu kuzisoma. 1. Taarifa ya...
Mapigano ya Wanakijiji Kugombea Ardhi Yasababisha Maafa Nchini Madagaska
Blogu ya L'Express Mada ilitoa taarifa kwamba kijiji kizima cha Andranondambo kilichoko Kusini mwa Madagascar kiliharibiwa [fr] kufuatia mapigano ya wanakijiji yaliyosababishwa na mzozo wa kumiliki ardhi. Vita vya wenyewe kwa wenyewe, ambayo ilidumu kwa siku tatu kati ya Mei 20-22, ilipoteza maisha ya wanakijiji wote. Akikumbuka tukio hilo, mmoja...
Gharama na Faida ya Kombe la Dunia Nchini Brazil
Blogu ya Daniel Bustos kutoka Colombia kuhusu uchumi wa Kombe la Dunia nchini Brazil na baada ya kugusia suala lisilo epukika la rushwa, inasema: Hatimaye, Brazil itatumika kama “panya” kwa mataifa ya Amerika ya Kusini ambayo yalikuwa na ndoto kuwa siku moja itaandaa tukio hili kubwa, itatumika kuuliza kama Brazil...
Maadili na Uwazi katika Makampuni Binafsi
Watu wanazidi kudai uwazi kwa uongozi wa serikali zao. Kwa kudai uwazi, watu wanachotaka ni kuthibitisha kuwepo kwa maadili katika shughuli za serikali. Lakini, je vipi kuhusu makampuni binafsi? Ingrid Kost anadhani [es] maadili ni muhimu kama tunataka ushirika endelevu: Mahitaji ya uwazi zaidi na kuongeza uwajibikaji kwa makampuni ya...
Sio Rahisi Ukiwa Mtu Mweusi Nchini Cuba
Habari mbaya kwa Wa-cuba wenye ngozi nyeusi au yenye mchanganyiko wa weusi na weupe ni kwamba hakuna taasisi huru za kisheria itawalinda kutelekezwa na serikali. Iván anaripoti kuwa watu wasio wazungu bado wanaendelea kubaguliwa nchini Cuba.
Trinidad na Tobago : Kutoka Serikali Moja hadi Nyingine
Nchi yetu haiwezi kuendelea kuuza nje ya nchi kazi zetu, rasilimali yetu, na watu wetu wenye ujuzi kuzifadhili sera za kigeni ambazo hazijachunguzwa wala kuwekwa wazi… Afra Raymond anasema kwamba mipango ya sasa ya serikali kwa serikali ni tisho la moja kwa moja kwa masilahi ya msingi ya Trinidad na...
Waziri Mkuu wa Zamani wa Malayasia Aitaka Boeing Kuwajibika kwa Ajali ya Ndege MH370
Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia Mahathir Mohamad ameitaka Boeing kuwajibika kufuatia tukio la kupotea kwa ndege ya Shirika la ndege la Malaysia yenye namba MH370. Hivi ndivyo alivyoandika kwenye blogu yake: Boeing ndiyo imetengeneza ndege hii. Boeing lazima waeleze inakuwaje njia zote za kuifuatilia mwenendo wa ndege hiyo ziweze...
Niger Yapata Kituo Chake cha Kwanza cha Reli Baada ya Kusubiri kwa Miaka 80
Aprili 7, Niger ilizindua katika mji mkuu wa Niamey kituo chake cha kwanza cha treni kuwahi [fr]. Mamlaka tayari ilikuwa na makadirio ya ujenzi wa kituo cha treni miaka 80 iliyopita lakini mradi kamwe haukuanzishwa. Tukio hilo litaanzisha ujenzi wa reli kati ya Niger, Benin, Burkina Faso na Côte d'Ivoire....