Habari kuhusu Picha kutoka Mei, 2014
PICHA: Watu 20,000 Waandaman huko Macau China Kupinga “Muswada wa Ulafi”
Muswada utampa mkuu wa serikali jimboni Macau, nchini China, kinga ya kushitakiwa kwa makosa ya kijinai wakati akiwa madarakani na ataaendelea kupata mshahara wake hata baada ya kuondoka madarakani.
Watu Wenye Ulemavu Kugombea Katika Uchaguzi wa Umoja wa Ulaya
"Sisi ni kikundi cha watu walioathirika, moja kwa moja au kwa namna moja au nyingine na ulemavu au lugha nyingine magonjwa nadra, tumeungana kwa lengo moja — nalo ni kuboresha maisha ya wale walioathirika."
PICHA: Waandamanaji Nchini Taiwani Wageuza Uzio wa Polisi kuwa Mapambo
Polisi waliweka uzio wa kuwapa tahadhari waandamanaji kuzunguka majengo ya serikali katika jitihada za kuwazuia waandamanaji kukusanyika. Wataiwani wakawajibu kwa kile kinachoonekana kuyageuza mabango hayo ya tahadhari kuwa mapambo.
Naijeria: Kampeni ya #Bringourgirlsback
Katikati ya mwezi Aprili, zaidi ya wasichana 200 wa shule walitekwa nyara kutoka shule ya sekondari iliyoko eneo la Chibok, Naijeria, kitendo kinachodaiwa kufanywa na Boko Haram, kundi la kigaidi lililoko katika eneo la kaskazini mwa nchi hiyo. Ingawa baadhi ya wasichana 57 wameweza kutoroka, bado wengine wengi wako...