Habari kuhusu Picha kutoka Juni, 2013
Mtu Mmoja Afariki Kwenye Maandamano Yanayoitikisa Brazil
Kijana mdogo aliuawa baada ya kugongwa na gari huko Ribeirao Preto na dazeni ya watu wengine walijeruhiwa pale waandamanaji walipokuwa wakikabiliana na polisi katika majiji ya Brasilia, Rio de Janeiro na Salvador kufuatia watu zaidi ya milioni moja kujitokeza katika mitaa ya majiji makubwa na madogo nchini kote Brazil katika maandamano makubwa ambayo hayakuwahi kushuhudiwa nchini humo kwa miongo miwili.
PICHA: Mamia Wakamatwa Nchini Brazil kwa Kupinga Ongezeko la Nauli za Mabasi
Polisi wanakabiliana kwa vurugu na kwa kutumia moshi wa machozi dhidi ya waandamanaji wanaopinga ongezeko la nauli ya usafiri wa umma katika maandamano ya yalioyodumu kwa siku ya nne mfululizo huko Sao Paulo. Maandamano haya ni sehemu ya Harakati za Kudai Usafiri wa Bure ambazo tayari zimeshasambaa katika miji mikuu mingine yote nchini Brazil.
Israeli: Waandamanaji Wakumbana na Ukatili wa Polisi Jijini Yerusalemu
Maandamano yaliyoandaliwa na vikundi vitatu vinavyohusiana na Vuguvugu la Israel la haki ya kijamii (#j14) yalifanyika jijini Yerusalemu mnamo Jumamosi usiku (Juni 8). Waandamanaji walidai kubatilishwa kwa uamuzi wa kuuza zaidi kiasi kikubwa cha hifadhi ya gesi wakati ni asilimia 12.5 tu ya mapato hayo yatakwenda serikalini kama kodi.
Wafanyakazi wa Sekta ya Afya Nchini Msumbiji Wagoma Kudai Maslahi
Wafanyakazi wa sekta ya afya nchini Msumbiji wamekuwa katika mgomo uliodumu kwa siku kumi na kusababisha kusimama kwa huduma katika vitengo vingi vya kutoa huduma za afya kote nchini humo. Mgogoro wao na serikali umetokana na madai yao ya kuboreshewa maslahi na mazingira ya kazi pamoja na kurekebishwa kwa gharama za chumba cha wagonjwa mahututi katika mahospitali yote nchini humo.