Habari kuhusu Habari Kuu
Serikali ya Nijeria yaifungia Twita baada ya mkanganyiko wa twiti ya rais iliyotishia matumizi ya nguvu kufutwa
Watumiaji wa twita nchini Naijeria kutoka kwenye makabila mbalimbali yalitumia majina ya Kiigbo kukuza alama habari ya #IamIgboToo kuonesha mshikamano wao na watu wa kabila la Igbo waliotishiwa na twiti ya Rais Buhari.
Matukio ya unyanyasaji wa kijinsia mtandaoni yaongezeka nchini Kenya
Katika mtandao wa intaneti nchini Kenya uliotawaliwa na wanaume, wanawake mara nyingi huwa walengwa wa matusi
Trinidad na Tobago yakaribia kurekebisha Sheria ya Fursa Sawa kutambua ushoga
Mijadala kuhusu hitaji la kubadili Sheria ya Fursa Sawa nchini Trinidad na Tobago imepamba moto baada ya benki kubwa nchini humo kuchukua hatua kubwa za kutambua haki za makundi mbalimbali.
MUBASHARA mnamo Mei 20: Tunachojifunza kuhusu Ulaya kupitia Shindano ya Eurovision
Shindano la Uimbaji la Eurovision linatuambia nini kuhusu siasa, taswira na maadili ya Ulaya? Ungana nasi mnamo Mei 20 kufahamu zaidi. Kipindi hiki kitaonesha mahojiano na washiriki wawili wa mwaka huu!
Mpango wa kutoa chanjo ya UVIKO-19 nchini Kenya waibua matabaka ya maskini na wasiojiweza
Wafanyabiashara na wanasiasa wanapata chanjo mapema wakati Wakenya masikini na wazee wakisimama kwenye foleni ndefu.
TAZAMA/SIKILIZA: Kupambana na miiko inayozuia utoaji mimba
Ulikosa matangazo mubashara ya kipindi cha Global Voices Insights cha Aprili 7 kuhusiana na masuala ya haki za kutoa mimba katika nchi tano? Tunakirudia hapa.
Baada ya Magufuli, Tanzania itarekebisha sheria kandamizi za maudhui ya mtandaoni?
Kanuni za maudhui ya mtandaoni nchini Tanzania zinatumiwa kuminya na kubana haki za matumizi ya mtandao na uhuru wa kujieleza. Je, kuapishwa kwa Rais mpya kutabadili sheria hizi kandamizi?
Kubadilika kwa Utawala Nchini Tanzania: Kutoka Rais Magufuli mpaka Rais Hassan
Kwa baadhi, Magufuli anakumbukwa kama "Mwana wa Afrika kweli kweli" mpigania haki za wa-Afrika aliyetanguliza maslahi ya Afrika mbele. Wengine wanamkumbuka kama Rais 'mpenda umaarufu" aliyepigania uzalendo — kuliko kingine chochote.
MUBASHARA mnamo Februari 10: Mazungumzo na Jillian C. York kuhusu kitabu chake kijacho “Silicon Values”
"Nani ana nguvu ya kuamua kitu gani kionekani na kipi kisionekane kwenye mtandao?"
Taarifa Za Ndani Zinasema; Wanafunzi wasiopungua 15 ‘Walitiwa mimba na wakufunzi’ katika chuo cha Polisi Msumbiji
Nyaraka hizo zilisema kuwa ujauzito huo ulitokana na mahusiano ya kingono baina ya wakufunzi bila kueleza kama mahusiano hayo yalikuwa ya hiari au lah.