GlobalVoices katika

Women & Gender

Hifadhi ya mada · 43 jumbe


Habari mpya Kuhusu Women & Gender

4 Mei 2013

Wabunge wa Ukraine Wataka Utoaji Mimba Upigwe Marufuku Kisheria

Soma makala hii.

Mapema mwezi Aprili, Wabunge watatu kutoka kambi ya Upinzani iitwayo“Svoboda” walipeleka mswada bungeni wenye lengo la kupiga marufuku utoaji mimba nchini Ukraine. Tetyana Bohdanova anataarifu mwitikio wa watumiaji wa mtandao kufuatia hatua hii ya Bunge la Ukraine.

2 Machi 2013

Wa-Mauritania Wapinga Udhalilishaji wa Viwanja vya Tahrir Square

صورة من الوقفة نشرها حساب موريتانيا اليوم على فيسبوك

Mwandamanaji akisema “Tunapinga Udhalilishaji” picha ya Jarida la “Mauritania Today” kwenye mtandao wa Facebook.


Siku ya Jumanne Februari 12, 2013, kikundi cha wanaharakati wa ki-Mauritania kiliandaa [ar] maandamano mbele ya Ubalozi wa Misri jijini Nouakchott, mji mkuu wa Mauritania, kupinga udhalilishaji wa kijinsia na ubakaji ambao wanawake wa ki-Misri wamekuwa wakikumbana nao kwenye viwanja vya Tahrir jijini Cairo.

Tukio hilo la maandamano liliratibiwa na “Etkelmi” (Sema kwa kiarabu) [ar - fr], Asasi Isiyo ya Kiserikali inayopambana na ubakaji nchini Mauritania. Mekfoula Brahim anawapa heshima wale wote walioshiriki maandamano hayo [ar]:

شكرا لكم يا مواطنو ا العالم على وقفتكم امام السفارة المصرية فى انواكشوط لدعم نساء مصر اللائى يمارسن حقهن فى التظاهر السلمى فى مصر وعلينا جميعا القيام بوقفة اخرى احتجاجا على دعم الارهاب علنا من طرف الكثيرين والتأصيل له فى ثقافتنا المنفتحة

Asante sana wananchi wote duniani kote kwa kuandamana mbele ya Ubalozi wa Misri jijini Nouakchott kuwaunga mkono wanawake wa Misri wanaotumia haki yao ya kuandamana kwa amani nchini Misri. Tuanze kuandaa mandamano mengine kuwapinga wale (wengi) wanaounga mkono ugaidi na wale wanaojaribu kuuchukua utamaduni wentu wa uwazi.

18 Februari 2013

Vurugu Zinazofadhiliwa na Serikali Nchini Angola

Mwanablogu Claudio Silva anaandika kwenye makala yake Africa Ni Nchi kwamba mtazamo wa kina juu ya vurugu zinazofadhiliwa na serikali (kufukuzwa watu mijini na kupigwa kwa waandamanaji) unahitajika ili kuelewa video mbili zilizosambaa sana mtandaoni na kuleta sintofahamu kubwa nchini (tazama habari maalumu za Global Voices). Anaandika “vurugu za Angola zimetoka ngazi za juu: Serikali”.

23 Januari 2013

Mwandishi wa Kike wa Yemeni Asumbuliwa kwa “Kutokuheshimu Dini”

Samia Al-Agbhari

Samia Al-Agbhari..mwandishi wa Yemeni anakabiliwa na mashambulizi ya kipropaganda. Picha iliwekwa kwenye mtandao wa Facebook na Afra Nasser

zaidi »

22 Januari 2013

“Wanasemaje Bamako?” Mazungumzo na Awa anayeishi Mali

Mazungumzo ya kila siku kwa njia ya skype(kwa Kifaransa)  kati ya Awa Traoré aliyeko Bamako na Anne Morin akiwa Ufaransa (kupitia anuani ya @annagueye)

Anne Morin na Awa Traoré wanabadilishana mawazo kuhusiana na maisha ya kila siku mjini Bamako, ujira usiokidhi mahitaji, gharama za maisha na hali ya kisiasa isiyotabirika wakati huu ambapo vita vinanukia nchini humo.

26 Disemba 2012

Korea Kusini: Mpango wa Kuwakutanisha Wenzi Wakwama

Mpango mpya kabisa wa kuwakutanisha wenzi kwa njia rahisi katika mkesha wa Krismas nchini Korea Kusini hatimaye ulijikuta ukishindwa kabisa baada ya waliojitokeza asilimia 90 kuwa ni wanaume. Inasemekana zaidi ya watu 20,000 walijiandikisha na hata polisi walikuwepo kufuatia uwezekano wa vitendo vya ngono za kulazimisha. Mtumiaji mmoja wa mtandaoalibainisha [ko] ukweli kwamba kosa lilikuwa ni kile alichokichagua mwanaume ndicho kilichosababisha kushindikana kwa zoezi hilo la kuwakutanisha wenzi.

23 Disemba 2012

Utambulisho wa Jamii ndogo ya Balkan

Face the Balkans subjects of stories

Picha ya mwonekano wa tovuti ya Balkans.

Waandishi vijana kumi na watano kutoka katika nchi zipatazo sita tofauti wametengeneza mfululizo wa masimulizi binafsi kuhusu masuala ya namna jamii zenye watu wachache (kwa mapana yake) zinavyoweza kuwakilishwa kutoka Bosnia na Herzegovina, Kosovo, Serbia, na Macedonia. Habari zinapatikana katika lugha za Kiingereza, Kijerumani, na Kifaransa katika mwonekano wa tovuti ya Balkans.

13 Novemba 2012

Watoto wa Mitaani Bangladesh Wakabiliwa na Unyanyasaji

Soma makala hii.

Jumla ya watoto wa mitaani nchini Bangladeshi wanakadiriwa kufikia 400,000. Karibu nusu ya idadi hiyo wanaishi katika Jiji la Dhaka. Asilimia kubwa ya watoto hao ni wasichana. Wasichana hao wa mitaani huishi katika mazingira yenye hatari nyingi hasa unyanyasaji na dhuluma nyingine.

12 Novemba 2012

Maelfu Watia Saini Pendekezo la Zawadi ya Nobel na Kusherehekea Siku ya Malala

Soma makala hii.

Mwanaharakati wa elimu mwenye umri wa miaka 15 -- Malala Yousufzai -- aliyepigwa risasi mnamo tarehe 9 Oktoba 2012 na wanamgambo wa TTP, anaendelea kupata nafuu japo polepole. Mnamo tarehe 10 Novemba, watu kote ulimwenguni walimpongeza Malala kama kielelezo kwa ajili ya wasichana wapatao milioni 32 ambao hawapati fursa ya kwenda shulen.

16 Oktoba 2012

Ghana: Vikwazo Vinavyowakabili Wanawake Kimaendeleo

Betty Mould Iddrisu, Jaji na Waziri wa Sheria wa Ghana, anaandika [fr] kwenye blogu ya pambazuka.org:

Kufikia ngazi za juu kabisa za utawala si rahisi, na hata unapopanda mpaka juu kabisa, bado unajikuta unakabiliwa na hisia za watu zenye uadui na watu wanakuwa na mashaka na uwezo wako, kwa sababu tu wewe ni mwanamke. Mwanamke akikamata madaraka ya juu humbidi kufanya kazi kwa bidii zidi kuliko mwanaume ili kuthibitisha uwezo wake, lakini bado hata akifanya hivyo anakumbana na uadui pamoja na mfumo unaomwona kuwa duni, iwe katika majukumu yake kama meneja na kiongozi, na hata katika mazingira yoyote ya kazi ambayo yanatawaliwa kwa kiasi kikubwa na wanaume.

Sehemu za Dunia

Nchi

Lugha