Habari kuhusu Safari
Video ya Kuonesha namna Mlima Ontake Ulivyolipuka
Mtu mmoja amethibitika kufa, wakati wengine wapatao hamsini wakiwa wamejeruhiwa vibaya, na wengine kumi hawajulikani walipo baada ya Mlima Ontake, ulio maarufu kwa ukweaji mlima, katikati ya Japani, kulipuka
Hali ya Kusikitisha Katika Kituo cha Magarimoshi cha Mumbai
Mwanablogu Antarik Anwesan anaelezea hali halisi ya kile kinachoendelea katika kituo cha magarimoshi cha Goregaon kilichopo Mumbai, India. Gari moshi lifanyalo safari za ndani liliondoka kituoni bila ya kutoa taarifa wakati abiria walipokuwa wakiharakisha kuingia. Kadri ya garimoshi lilivyoongeza mwendo, watu wawili walianguka kupitia mlangoni, chupuchupu kupoteza maisha. Taarifa ya...
Sababu za Kusafiri Mara Moja Moja
Kwenye blogu yake iitwayo Historias de una mujer lobo (Hadithi ya mbwamwitu wa kike), Natalia Cartolini anatafakari kuhusu sababu za kwa nini kusafiri kunaweza kuwa na faida kama, kwa maoni yake, “kutembelea maeneo mapya au kukutana na watu wapya wenye mtazamo mwingine ni muhimu wakati wote. Haijalishi kama unatoka kutembea...
Je, Ujumbe wa Shirika la Ndege la Singapore Baada ya Ndege MH17 Kuanguka Haukuwa wa Kiugwana??
Baada ya habari kufahamika kwamba ndege ya Shirika la Ndege la Malaysia MH17 imeanguka mashariki mwa Ukraine, Shirika la Ndege la Singapore liliweka ujumbe huu kwenye mtandao wa Facebook na Twita: Customers may wish to note that Singapore Airlines flights are not using Ukraine airspace. — Singapore Airlines (@SingaporeAir) July...
Wamalaysia kwenye Ndege MH17 Iliyoanguka: “Bila Kujali Utaifa, Tuko Pamoja Kuomboleza””
Ndege ya Shirika la Malaysia MH17, iliyokuwa ikisafiri kutoka Amsterdam kwenda Kuala Lumpur, imeanguka mashariiki mwa Ukraine Alhamisi jioni. Ndege hiyo ilikuwa na abiria 298 pamoja na wafanyakazi
Udhalilishaji wa Kijinsia wa Watoto Wanaotalii Asia ya Mashariki
Mradi wa Nguzo ya Kuokoa Utoto, uliobuniwa na serikali ya Australia, umezinduautafitiukosefu wa msaada wa kijamii, elimu, furasa na ulinzi” kwa kuendelea kwa vitendo vya kuwadhalilisha watoto. Utafiti huo pia umeonyesha namna kusafiri na utalii “ni hatari nyingine inayochangia shida za kudhalilishwa zinazowakumba watoto.” Utafiti huo ulihusisha nchi za Thailand,...
Puerto Deseado, Ahera ya Pwani
Kwenye blogu yake Viajes y Relatos, Laura Schneider anasimulia uzoefu wake alipotembelea Puerto Deseado, mji ulioko kwenye Jimbo la Santa Cruz, Ajentina. Katika siku yake ya sita ya safari yake ya kupiga picha, alitembelea na kupiga picha za mji huo mzuri katika maeneo ya karibu: Yendo por la ruta 3,...
Sio Rahisi Ukiwa Mtu Mweusi Nchini Cuba
Habari mbaya kwa Wa-cuba wenye ngozi nyeusi au yenye mchanganyiko wa weusi na weupe ni kwamba hakuna taasisi huru za kisheria itawalinda kutelekezwa na serikali. Iván anaripoti kuwa watu wasio wazungu bado wanaendelea kubaguliwa nchini Cuba.
Namna ya Kutafuta Chumba cha Kupanga Nchini China
Chengdu Living anawafundisha wasomaji wake namna ya kutafuta chumba cha kupanga nchini China bila kwenda kwa dalali kwa kutoa mwongozo wa hatua tano.
Waziri Mkuu wa Zamani wa Malayasia Aitaka Boeing Kuwajibika kwa Ajali ya Ndege MH370
Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia Mahathir Mohamad ameitaka Boeing kuwajibika kufuatia tukio la kupotea kwa ndege ya Shirika la ndege la Malaysia yenye namba MH370. Hivi ndivyo alivyoandika kwenye blogu yake: Boeing ndiyo imetengeneza ndege hii. Boeing lazima waeleze inakuwaje njia zote za kuifuatilia mwenendo wa ndege hiyo ziweze...