Habari kuhusu Teknolojia kutoka Aprili, 2010
Poland: Utata Kuhusu Sehemu Atakayozikwa Rais wa Poland
Tangazo la leo kuwa rais wa Poland na mke wake, waliofariki katika ajali mbaya ya ndege huko Smolensk Jumamosi iliyopita, watazikwa katika Kasri la Wawel huko Krakow limezua utata mwingi. Sylwia Presley anatafsiri mitazamo ya baadhi ya wanachama wa Facebook wa kiPoland.
Tunisia: Wanablogu wa Tunisia Wazungumza Kiingereza
Wanablogu wa Tunisia walizoea kuepuka kutumia Kiingereza (lugha ya tatu nchini mwao), na badala yake waliandika kwa Kiarabu (na wakati mwingine kwa lahaja za Tunisia) au Kifaransa. Lina Ben Mhenni anazitupia macho baadhi ya blogu zinazoandikwa kwa lugha ya Kiingereza.