· Disemba, 2009

Habari kuhusu Teknolojia kutoka Disemba, 2009

China na Iran: #CN4Iran

  28 Disemba 2009

Jana, maelfu ya Wa-Irani waliingia mitaani ili kupinga dhidi ya utawala wa kiimla. Maandamano hayo yaliwakumbusha watu wa China juu ya vuguvugu la demokrasi la Tiananmen la 1989 na watumiaji wa Ki-China wa twita wanatumia alama ya #cn4iran ili kuonyesha mshikamano na wenzao wa Irani.

Poland: Blogu Zataka Malipo

  16 Disemba 2009

Wasomaji wa blogu zinayoongoza za lugha ya Kipolish ni lazima wameshangazwa kuona kivinjari skrini mpya ya ukaribisho kwenye moja ya tovuti zinazopendwa: Imetangaza kwamba, kuanzia Disemba 14, 2009, kupatikana kwa blogu hiyo hakuta kuwa bila ya gharama. Jakub Gornicki anaandika kuhusu habari hiyo.

Indonesia: Sarafu za Kudai Haki

  8 Disemba 2009

Raia wa mtandaoni (Netizens) wamezindua kampeni ya kukusanya fedha zilizo katika muundo wa sarafu ili kumuunga mkono Prita Mulyasari, mama wa nyumbani raia wa Indonesia aliyeandika malalamiko yake mtandaoni dhidi ya hospitali iliyotoa huduma mbaya, na ambaye alipatikana na hatia na mahakama moja ya kosa la "kuchafua jina" la hospitali hiyo binafsi.