The Global Voices Lingua project hopes to bring GV content to new linguistic audiences - Details

Also in:

Religion Hifadhi ya mada

Kiungo cha RSS kwa Religion

2009-11-14

Marekani: Mauaji ya Fort Hood Yasababisha Kumulikwa kwa Waislamu Walio JeshiniVideo post

Shambulizi la upigaji risasi la kushtukiza lililofanywa na mwanajeshi wa Jeshi la Marekani, Meja Nidal Malik Hassan, na kusababisha vifo vya watu 13 na kujeruhi wengine 31 katika kambi ya kijeshi ya Fort Hood, jimbo la Texas, kwa mara nyingine limesababisha Waislamu nchini Marekani kumulikwa - hasa wale wanolitumikia jeshi.

2009-11-04

Georgia: Aibu Katika Kanisa la Orthodox

Katika nchi inayofuata dini zaidi kwenye maeneo ya kusini mwa Caucasus ambako mkuu wa Kanisa la Orthodox (madhehebu ya Kanisa la zamani au kihafidhina) anaweza kuhamasisha ongezeko la watoto, kukosoa watumishi wa kanisa bado ni mwiko. Kuwatania, hata hivyo, ni jambo baya zaidi na lililojaa hatari.

2009-10-25

Marekani: Wanandoa wa rangi tofauti wanyimwa cheti cha ndoa

Juma lililopita huko Hammond, Louisiana, wapenzi wawili walituma maombi ya kibali cha kufunga ndoa na walikataliwa kwa misingi ya rangi zao tofauti. Afisa wa kutathmini na kuandikisha nyaraka (Muamuzi wa Amani) alidai kuwa “ndoa baina ya watu wa rangi hazidumu” na alisema kuwa anafanya hivyo “kwa ajili ya watoto.”

2009-09-26

Marekani: Stempu ya Iddi Yachochea Chuki Huko Tennessee

Barua pepe yenye madai ya uongo kuwa Rais Obama ametoa stempu mpya kuadhimisha sikukuu ya Waislamu Eid al-Fitr imemfikia Meya wa Tennessee ambaye aliisambaza kwa wafanyakazi wake na waasa waisusie stempu hiyo.

2009-07-24

Nchi za Kiarabu: Homa ya Mafua ya Nguruwe Yaendelea

Homa ya mafua ya nguruwe au H1N1 bado inatawala vichwa vya habari vya magazeti katika nchi za Kiarabu kwani wagonjwa wapya wanaendelea kugunduliwa na mamlaka za afya na kutangazwa katika vyombo vya habari kila siku. Huu ni muhtasari wa yale wanayoongea wanablogu huko Bahrain, Jordan, Misri na Syria.

2009-05-25

Saudi Arabia: Je, mafua ya nguruwe yatatishia Hija?

Kila mwaka mamilioni ya Waislamu hukusanyikia Maka kuhiji, moja ya nguzo tano za Uislamu. Je, msimu wa hija ya mwaka huu utatishiwa na homa ya mafua ya nguruwe? Wanablogu wanayo maoni ya kusema.

2009-03-24

Papa Nchini Kameruni (2): Wazee Wa Kanisa, Upotofu na Siasa

Ziara ya kiongozi wa Kanisa La Katoliki nchini Kameruni mwezi huu wa Machi 2009 imepelekea baadhi ya mabloga wa Kikameruni kuelekeza tochi zao kwenye matokeo ya kisiasa (kama yapo) yatakayotokana na ziara hiyo ya Papa nchini humo.

Papa Nchini Kameruni (1): Utata wa Safisha-safisha Jijini Yaounde

Papa Benedikti wa XVI anazuru Kameruni kuanzia tarehe 17 mpaka tarehe 20 Machi 2009. Ziara hii imepelekea serikali kuchukua hatua kali za usafi, ambazo zimezua utata mkubwa katika ulimwengu wa blogu nchini Kameruni.