Middle East & North Africa
Kwa mujibu wa Kian majeshi ya usalama yaliwashambulia waandamanaji katika viwanja vya hafteh tir mjini Teheran na kuwajeruhi watu kadhaa.



Leo ni Kumbukumbu ya 20 ya kuanguka kwa Ukuta wa Berlini, kizingiti madhubuti cha kiusalama ambacho kiliwahi kuligawa jiji la Berlini katika pande mbili za Mashariki na Magharibi huko Ujerumani. Leo tunaonyesha baadhi ya picha za video zinazotoka pande mbalimbali za dunia zinazopandishwa ili kusherehekea siku hii na nini ukuta huo ulimaanisha siyo Ujerumani tu bali duniani kote.
2009-11-06

Upande wa upinzani wa Vuguvugu la Kijani nchini Irani mnamo tarehe 4 Novemba uliendesha maandamano makubwa ambapo maandamano hayo yalikabiliwa na matumizi makubwa ya nguvu ya kuyazuia yaliyofanywa na vikosi vya usalma. Kama ambavyo sasa inatarajiwa, uandishi wa habari wa kiraia nchini Irani haukukosa kitu kwani ulirekodi 'historia' hiyo kupitia simu zao za mikononi.
2009-11-04
Kwa mujibu wa Kian majeshi ya usalama yaliwashambulia waandamanaji katika viwanja vya hafteh tir mjini Teheran na kuwajeruhi watu kadhaa.
2009-11-03
2009-10-26
“Trinidad na Tobago ni kisiwa tajiri na nchi inayoendelea tajiri kwa mafuta na gesi asilia. Lakini pia tunashuhudia madhara mabaya ya maendeleo ya haraka kwenye nyanja za viwanda katika visiwa vyetu. Hii ni fursa ya sauti za wanawake kusikika”: Attillah Springer anajihusisha na kampeni ya hali ya hewa 350.
2009-10-12
Ripoti ya MISNA (Shirika La Kimataifa la Habari La Wamisionari) iliyochapishwa tarehe 25 Septemba inaeleza kuwa maandamano makubwa ya upinzani yalifanyika mjini Labe, jiji la pili kwa ukubwa nchini Guinea, dhidi ya Mkuu wa Nchi Mwanajeshi, Kapteni Moussa Dadis Camara.
2009-09-16
Wakati machafuko yalipoitingisha Kampala, mji mkuu wa Uganda, kwa siku ya pili, wanablogu na watumiaji wa intaneti waliungana ili kuupasha ulimwengu habari.
2009-06-17

Zaidi ya watu 100,000 waliandamana mjini Tehran Jumatatu iliyopita ili kumuunga mkono mgombea urais mwanamageuzi, Mir Hussein Mousavi pamoja na madai yake ya kuataka kubatilishwa kwa matokeo ya uchaguzi ambayo yalimtangaza rais aliye madarakani Mahmoud Ahmadinejad kama mshindi katika uchaguzi wa tarehe 12 Juni. Damu ilimwagika mwishoni mwa maandamano hayo. Watu wapatao 7 walipoteza maisha yao.