Habari kuhusu Siasa kutoka Februari, 2015
Asasi ya Kiraia Inayofuatilia Bunge Yawaunganisha Wabunge Wanawake na Wananchi wa Uganda
Asasi ya Kiraia ya Parliament Watch Uganda iliandaa mjadala wa kujadiliana na wabunge wanawake kwenye mtandao wa Twita kuhusu mada 'Kuwafanya Wanawake Wathaminiwe Kwenye Shughuli za Kibunge'.
Mradi wa Video Waelezea Mapambano ya Kimaisha ya Watu wa Papua ya Magharibi
"Hizi ni habari tofauti na zile za mgogoro uliopo: Harakati za kupata elimu, mazingira, usawa na utu."
Ufisadi Uliofanywa na Makampuni Makubwa Katika Kupambana na Ebola Nchini Sierra Leone
Makampuni matano nchini Sierra Leone yanasemekana kutumia fedha zilizokusudiwa kupambana na Ebola kwa njia za kifisadi: Haya hapa makampuni matano yaliyokuwa yameingia mikataba mikubwa ya kusambaza vifaa na kutoa huduma katika kupambana na ugonjwa wa Ebola nchini Sierra Leone kama yalivyoorodheshwa kwenye Taarifa ya Ukaguzi ya Fedha za Kupambana na...
2015 Mwaka wa Kufanyika Chaguzi Huru na Haki Barani Afrika
Wekesa Sylvanus anataraji kwamba 2015 utakuwa mwaka wa chaguzi huru na haki barani Afrika: https://wekesasylvanus.wordpress.com/2015/02/18/will-2015-be-a-year-of-free-and-fair-elections-in-africa/ Tangu kurejeshwa kwa mfumo wa demokrasia ya vyama vingi barani Afrika, ushindani nyakati za uchaguzi umekuwa suala la kufa na kupona kwenye nchi nyingi za ki-Afrika. Chaguzi barani Afrika ni suala lenye hatari zake na...
Chemsha Bongo: Je, Uko Kwenye Hatari ya Kugeuka Gaidi?
Chemsha bongo hii imeandaliwa kwa kutumia utafiti unaofanywa na serikali ya Marekani unaotumiwa kuwabaini watu wenye hatari ya kuwa magaidi au jamii zilizokwenye hatari ya kukumbatia na kuleta itikadi zenye msimamo mkali.
Je, Kuahirishwa kwa Uchaguzi Mkuu Naijeria Kunatokana na Sababu za Kiusalama?
Jeshi la Nigeria litaendesha operesheni maalum ya wiki sita dhidi ya Boko Haram ili"kuepusha kuingiliwa na shughuli za uchaguzi." Baadhi ya watu wanatilia shaka kuwa, kuahiririshwa kwa uchaguzi ni mkakati wa kisiasa.
Hofu ya Yaliyotokea? Likizo ya Rais Mpya wa Zambia Yaibua Mjadala wa Afya Yake
Raia wa Zambia wanajiuliza maswali kuhusu afya ya Rais Lungu, pamoja na cheti cha afya kuonesha yu mzima, kufuatia likizo yake majuma mawili tu tangu ashike madaraka kumrithi Michael Sata, aliyefariki akiwa madarakani.
GV Face: Maandamano Yazuiliwa na Waasi wa Houthi Nchini Yemen
Yemen iko kwenye mzozo wa kisiasa, bila kuwa na rais na serikali, tangu wanamgambo wa Houthi kuangusha taasisi za kiserikali na kuiteka ikulu kwenye mji mkuu wa Sanaa
Raia wa Masedonia Watumia Sheria ya Uhuru wa Habari Kupinga Sheria Mpya ya Wafanyakazi
Baadhi ya wafanyakazi wasio na mikataba y kudumu pamoja na wale walio na mwajiri zaidi ya mmoja walizuiwa kupokea mishahara yao ya mwezi Januari kwa mujibu wa sheria mpya za kodi na utoaji wa ada. Waandamani wana lengo la kuweka bayana namna serikali isivyokuwa na utaratibu mzuri wa kutekeleza sheria hizi.
Boko Haram Yaua Watu Wasiopungua 81 Huko Fotokol, Cameroon Kaskazini
Mnamo Februari 4, Boko Haram walifanya shambulio baya kwenye mji wa Fotokol Kaskazini mwa Cameroon, baada tu ya kuvuka mpaka wa Naijeria. Mamia wa raia wanahofiwa kupoteza maisha 81 wamethibitika kufa na Wizara ya Ulinzi. Shirika la Haki za Binadamu nchini humo linaamini kwamba karibu watu 370 wameuawa. Mashuhuda wa...