Habari kuhusu Siasa kutoka Septemba, 2014
Waandamanaji Wanaodai Demokrasia Wageuza Hong Kong Kuwa Bahari ya Miamvuli
Yakiwa yamepewa jina la utani la "mapinduzi ya miamvuli" na baadhi ya vyombo vya habari, maandamano ya Hong Kong yatawaliwa na waandamanaji wanaojikinga na mabomu ya kutoa machozi kwa kutumia miamvuli.
Polisi wa Hong Kong Wawapiga Mabomu ya Machozi Waandamanaji Wanaodai Demokrasia
Polisi walipambana na waandamanaji baada ya maandamano ya kukaa katikati ya jiji la Hong Kong kudai uchaguzi wa demekrasia halisi.
Vyombo vya Habari Vyaususia Wimbo wa Kupigania Uhuru Ulioimbwa na Msanii Maarufu Nchini Macedonia
Msanii maarufu wa Macedonia wa miondoko ya kufoka foka amejikuta akipoteza umaarufu baada ya kuachia ‘kibao’ kinachojadili masuala ya uhuru wa habari nchini Macedonia.
Kimbia! Waislamu Wanakuja!
Mtazamo wa vyombo vikuu vya habari mara nyingi unaonesha “Waislamu” wenye sura moja kubwa, ambayo haikosi kuwa na ghasia. Kwenye kichekesho hiki kisicho na maana yoyote, Mchekeshaji wa ki-Pakistani Sami Shah anakuletea makundi makuu ya “waislamu”.
Wanabogu wa Togo Wamtania Rais Kufuatia Ujumbe wa Bango Barabarani
Mtu mmoja alitaka watu wajue kwamba alikuwa na shukrani kwa ukarimu wa Rais wa Togo Faure Gnassingbé. Wiki hii, bango kubwa liliwekwa jijini Lomé, Togo kusifia kitendo cha Rais kutoa chakula cha mchana kwa watoto. Bango hili linaloonekana hapa chini lina maneno haya kwa lugha ya Kifaransa:” Asante sana Baba Faure...
Jinsi Wanablogu Walifikia Gerezani kwa Kuandika Kuhusu Haki za Binadamu Nchini Ethiopia
Melody Sundberg anachambua uhuru wa kujieleza nchini Ethiopia baada ya wanablogu wa Ethiopia waliokamatwa kukaa siku 100 gerezani: Ethiopia ina idadi ya watu 94,000,000 na ni nchi ya pili yenye wakazi wengi katika bara la Afrika. Hata hivyo, hailingani na mahojiano ya Endalkhachew Chala kupitia Global Voices, kuwa na gazeti...
Habari Mpya za Mgogoro wa Kisiasa Lesotho Kupitia Twita
Mfuatilie @nthakoana (Nthakoana Ngatane) kupata habari mpya zinazohusu mgogoro wa kisiasa nchini Lesotho. Nthakoana Ngatane ni mwandishi, msemaji, mwimbajii, mwigizaji na mwakilishi wa SHirika la Habari la Utangazaji la Afrika Kusini nchini Lesotho. Mnamo tarehe 30 Agosti 2014, Waziri Mkuu wa Lesotho Tom Thabane alidai kulikuwa na jaribio la kumpindua...
Je Kulikuwa na Jaribio la Mapinduzi Nchini Lesotho?
Sikiliza sauti inayoelezea kile hasa kinachoendelea nchini Lesotho kufuatia madai ya mapinduzi ya kijeshi: Waziri mkuu amekimbilia nchini Afrika Kusini na anasema ni mapinduzi ya kijeshi. Jeshi la Lesotho linasema sio mapinduzi. Siasa zinazua utata. African Defence Review inazungumza na KRISTEN VAN SCHIE wa SADC na mwandishi DARREN OLIVIER kuuliza...