Habari kuhusu Siasa kutoka Juni, 2013
Raia wa Myanmar Wachukizwa na Mashambulizi Dhidi ya Wahamiaji Wenzao Nchini Malasia.
Vurugu za kikabila nchini Mynmar inaonekana kusambaa hata katika nchi za jirani.. Baadhi ya wahamiaji wa Mynmar wa jamii ya budha wanaoishi nchini Malasia wiki chache zilizopita ambapo watu wengi wanaamini kuwa mashambulia hayo yanahusiana mvutano wa kimakabila na kidini unaoendelea nchini Myanmar. Mwitikio wa awali wa serikali ya Myanmar wa kukanusha matukio haya uliwakasirisha watumiaji wengi wa mtandao.
Israeli: Waandamanaji Wakumbana na Ukatili wa Polisi Jijini Yerusalemu
Maandamano yaliyoandaliwa na vikundi vitatu vinavyohusiana na Vuguvugu la Israel la haki ya kijamii (#j14) yalifanyika jijini Yerusalemu mnamo Jumamosi usiku (Juni 8). Waandamanaji walidai kubatilishwa kwa uamuzi wa kuuza zaidi kiasi kikubwa cha hifadhi ya gesi wakati ni asilimia 12.5 tu ya mapato hayo yatakwenda serikalini kama kodi.
Bajeti ya Bangladesh: Maoni na Uchambuzi
“Bajeti ya kifahari lakini mpango duni?” Raia wa kawaida anatoa maoni na kuichambua bajeti ya hivi karibuni ya Bangladesh kwa mwaka wa fedha 2013-2014.
Misri Inavyopoteza Miji ya Kihistoria
Cairoobserver atoa wito [ar] kwa wakaazi wa Misri kupitia mtandao wa
Misri: Wafanyakazi wa Asasi Zisizo za Kiserikali Nchini Misri Wafungwa Jela
Kuhukumiwa kwa wafanyakazi wa ki-Misri na kigeni wanaofanya kazi katika asasi zisizo za kiserikali (NGO) kifungo cha hadi miaka mitano jela, kumesababisha hasira katika mitandao ya kijamii na katika maeneo mengine. Hatua hiyo imeonekana kama onyo kwa mashirika ya kutetea haki za binadamu na yale yanayokuza demokrasia.
Je, Italia Iko Tayari kwa Waziri Aliyezaliwa Afrika?
“Je, Italia iko tayari kwa Waziri wa Serikalki aliyezaliwa Afrika?,” Donata Columbro anauliza: Miezi miwili baada ya uchaguzi wa hivi karibuni, Italia ina serikali mpya. Na Cécile Kyenge, mwenye umri wa miaka 48, daktari wa upasuaji macho na raia wa Italia aliyezaliwa Kongo, ni Waziri mpya wa Ushirikiano katika baraza la mawaziri la Waziri...
Kukamatwa kwa Mwandishi wa Habari wa Kimasedonia Kwachochea Maandamano
Waandishi wa habari wa Kimasedonia walikusanyika [tazama video na soma nakala] mbele ya Mahakama ya Makosa ya Jinai hivi leo katika mji mkuu Skopje kupinga kukamatwa kwa mwenzao, Tomislav Kezarovski, kwa mujibu wa maandishi haya [en] yaliyoandikwa katika ukurasa wa kundi la Kimasedonia kwenye mtandao wa Facebook yaliyopewa kichwa cha habari cha “Waandishi wa...
Ukatili wa Polisi Nchini Macedonia: Miaka Miwili Baadae
Siku ya Alhamisi, Juni 6, katika kituo cha Skopje, Vuguvugu la Kupinga Ukatili wa Polisi litatimiza miaka miwili baada ya mauaji ya Martin Neshkovski, ambayo yalisababisha maandamano makubwa katika ngazi za chini kabisa nchini Macedonia katika majira ya joto ya 2011. Tukio la Facebook [mk] kuhusu ibada ya kumbukumbu linaeleza: Siku ya Alhamisi,...
Iran: Utani Kuhusu Mdahalo wa Urais
Raia wa mtandaoni kadhaa walitwiti kuhusu mjadala wa pili wa rais na waliwakejeli wagombea. Potkin Azarmehr alitwiti “Wagombea urais wanaweza kuombwa kucheza muziki.”
Uganda: Hatimaye Magazeti Yaliyofungiwa na Polisi Yafunguliwa
Uganda imeruhusu magazeti mawili kufunguliwa tena baada ya msuguano uliodumu kwa siku 11 kati ya serikali na vyombo vya habari juu ya barua yenye waliyoipata ambayo iliyoonyesha njama ya kumtayarisha mtoto wa kwanza wa Rais Yoweri Museveni kumrithi kiongozi huyo aliyedumu kwa miaka 27.