· Februari, 2013

Habari kuhusu Siasa kutoka Februari, 2013

Mgomo wa Nchi Nzima Wamshitua Rais wa Malawi

Rais wa Malawi Joyce Banda atupilia mbali shinikizo la kujiuzulu mara baada ya mamia ya maelfu ya wafanyakazi wa umma kuandamana kwa wiki mbili kuishinikiza serikali kuongeza mishahara, hali iliyopelekea kufungwa kwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Malawi na kusababisha hali ya taharuki mahospitalini na mashuleni.

Udhaifu wa Watawala wa Afrika unajionesha Mali?

Ousmane Gueye katika tovuti ya Mondoblog anaandika [fr] kuhusu kuchelewa kupeleka vikosi vya kijeshi kasikazini mwa Mali: Kama tungekuwa tunasaiili matokeo ya watu wenye amani na huru kuingilia kati hali ya mambo nchini Mali, basi ni wazi kuwa kwa kuchelewa kupeleka vikosi vya ulinzi, nchi za Afrika zimewakosea wananchi wa Mali...