Habari kuhusu Siasa kutoka Januari, 2013
Pasipoti za Kidiplomasia kwa Viongozi wa Kidini nchini Brazil?
Wizara ya Mahusiano ya Kimataifa ilitoa pasipoti za kidiplomasia kwa viongozi wa kanisa la kiinjili liitwalo World Church of the Power of God, hatua ambayo imewasha majadiliano makali kuhusu dhana ya nchi kutokuwa na dini kama inavyotamkwa katika katiba ya Brazili.
Rais wa Chadi Awateua Wanawe Kushika Nafasi Nyeti
Djamil Ahmat anaripoti kuwa rais Déby wa Chadi amemteua mwanae wa kiume Mahamat Idriss Déby, 24, kuwa brigedia jenerali [fr] pamoja na maafisa wengine wanne. Tchadanthopus anaongeza kuwa mwanae mwingine Zackaria Idriss Deby alisemekana kukabidhiwa umakamu wa rais [fr] nafasi ambayo inampa madaraka yote wakati baba yake anapokuwa nje ya...
Mwaka Mpya na Mienendo ya Zamani Nchini Bahrain
Wakati nchi mbalimbali ulimwenguni kote zikiukaribisha mwaka mpya kwa fataki na shamrashamra, serikali ya Bahraini iliandaa utaratibu wa aina yake kwa waandamanaji nchini humo. kwa bahati, watumiaji wa mtandao wa intaneti walikuwa tayari, kuonesha na kuweka kumbukumbu ya baadhi ya matukio kwa ajili ya kushuhudiwa na sehemu nyingine yote ya ulimwengu.
Waandamanaji wa Hangari Wafunga Daraja, Wanafunzi Watatu Watiwa Nguvuni.
Harakati za maandamano ya wanafunzi zinaendelea nchini Hangari. Usiku wa Jumatano, waandamanaji walizingira daraja la Budapest na wanafunzi watatu waliishia kuwekwa kizuizini na polisi.