· Mei, 2011

Habari kuhusu Siasa kutoka Mei, 2011

Uganda: Polisi Wawanyunyizia Waandamanaji Rangi ya Waridi

Polisi wa Uganda wameikabili kampeni inayoendelea kwa mwezi mmoja sasa ya Kutembea Kwenda Kazini kwa kuwanyunyuzia waandamanaji moshi wa machozi na risasi sa moto. Wakati wa maandamano siku ya Jumanne, walitumia mbinu mpya, ya kuwashambula waandamanaji waliokuwa wakijaribu kuandamana kuelekea viwanja vya katiba katikati ya jiji la Kampala kwa maji yaliyochanganywa na uji wa rangi ya waridi.

Singapore: Wanablogu Waikosoa Ilani ya PAP

  12 Mei 2011

Chama kinachotawala Singapore, People’s Action Party (PAP), kilitoa ilani yake ya uchaguzi tarehe 17 aprili, 2011, ambayo mara moja ilikosolewa na wanablogu wengi kwa “kutokuwa wazi”. PAP tayari kimekuwa madarakani kwa miongo mitano. Uchaguzi mkuu nchini humo umefanyika tarehe 7 Mei.

Nepal: Mwanzo wa Mapinduzi ya Facebook?

  10 Mei 2011

Pradeep Kumar Singh anaweka picha na habari za kampeni ya hivi karibu ni ya Facebook iliyopewa jina la “Jitokeze. Simama. Ongea. Vinginevyo, kaa kimya. Takriban vijana 400 wa Nepali walijitokeza sehemu ya Maitighar Mandala tarehe 8 Mei, 2011 na kudai katiba mpya.

Senegal: Harakati za “Imetosha Sasa Basi”: Kwanza Kwenye Mtandao, Na Sasa Ikulu

Wakati vuguvugu la mapinduzi likiendelea Uarabuni, matukio kadhaa ya vijana wenye hasira yamezuka katika tovuti za Senegal. Tangu mwanzoni mwa mwezi wa tatu, uanaharakati huo umeachana na ulimwengu wa mtandao na kundi linalojiita “Y'en a marre” (Imetosha Sasa Basi) sasa limegeuka na kuwa alama ya vuguvugu la upinzani. Founded in January 2011, Y’en a marre arose from frustration built up during power cuts that brought Senegal to a standstill. The group hails from the Dakar suburbs and is led by several local rappers, including Fou Malad, Thiat (from the group Keur Gui) and Matador.