Habari kuhusu Siasa kutoka Disemba, 2010
Urusi: Habari ya Putin-Berlusconi Kwenye WikiLeaks
Kwenye The Daily Beast, Julia Ioffe anatoa maoni juu ya masuala yaliyowekwa wazi katika Wikileaks kuhusu uhusiano kati ya Waziri Mkuu wa Urusi na mwenzake wa Italia Silvio Berlusconi.
Mashariki ya Kati: Mawasiliano ya Siri Ambayo Sio Siri ya Ubalozi wa Marekani
Wakati vyombo vya habari vikuu Uarabuni vimeyapokea kwa bega baridi mawasiliano ya siri ya Balozi za Kimarekani, wanablogu na watumiaji wa Twita kutoka Mashariki ya Kati walipata habari zinazohitajika sana kwa uchambuzi.
Brazil: Leo Rais, Kesho Mwanablogu
Rais wa Brazil anayeondoka madarakani Luis Inácio Lula da Silva (Lula) alihojiwa na wanablogu wapenda maendeleo (au wenye mlengo wa kati kuelekea kushoto) kwa mara ya kwanza wiki hii, tukio ambalo limechukuliwa na wengi kama hatua muhimu katika msukumo uliopo unaotaka mfumo wa habari wa kidemokrasia zaidi nchini Brazil.