Habari kuhusu Siasa kutoka Aprili, 2010
Irani: Je Blogu Zimepoteza Umaarufu Tangu Uchaguzi
Je uchaguzi wa rais ulibadili jinsi nyenzo za uanahabari wa kiraia zinavyofanya kazi nchini Irani? Wanablog wa Irani kumi na moja na wandishi wa habari wanaowakilisha sehemu tofauti za misimamo ya kisiasa wamejibu dodoso kuhusu mabadiliko uanahabari wa kiraia nchini Irani tangu Uchaguzi.
Colombia: Mockus na Fajardo Waungana kwa Ajili ya Uchaguzi wa Rais
Mameya wawili wa zamani wa amajiji 2 makubwa zaidi nchini Kolombia wameunganisha majeshi kugombea katika uchaguzi wa rais wa Mei 30 kwa tiketi moja. Umoja huu mpya wa Chama cha Kijani umepokewa vizuri na watumiaji wa vyombo vya habari vya kijamii, ambo ni sehemu kubwa ya mkakati wa kampeni.
Guatemala: Hadithi ya Maziwa Mawili, Macaws na Malkia
Wanaharakati wa mazingira wana hofu kuhusu kuendelea kuchimbwa mafuta katika Hifadhi ya taifa ya Laguna del Tigre, ambayo ni moja ya maziwa ya asili nchini guatemala ambalo lina utafuti wa mazingira na ambalo liko hatarini.
South Africa: Mauaji ya kiongozi wa Afrikaner Resistance Movement
Usiku wa Tarehe 3, Aprili 2010, kiongozi wa kundi la watetezi wa Waafrika Kusini wenye asili ya Udachi (Afrikaans Weerstandsbeweging (AWB), au Afrikaner Resistance Movement), Eugene Terre'Blanche, aliuawa. Je raia wa dijitali wana nini cha kusema kuhusu kifo chake na mustakabali wa mahusiano baina ya watu wa rangi tofauti nchini Afrika kusini?
Kirigistani: Mapinduzi “Yaliyowekwa kwenye Kumbukumbu”
Mnamo tarehe 6 April, nchi ya Kirigistani ilikumbwa na maandamano makubwa ya kupinga utawala ambayo hatimaye yaliing'oa serikali pamoja na kusababisha vifo vya watu wengi. Pamoja na kwamba intaneti haikushika usukani katika kuhamasisha maandamano hayo, imetumika sana katika kuhifadhi kumbukumbu za kina za maandamano hayo.
Brazili: Ulimwengu wa blogu waunga mkono sheria ya kuzuia ufisadi
Muswada wa sheria kwa ajili ya kuwazuia wanasiasa ambao wamewahi kutenda makosa makubwa ya jinai ili wasigombee nafasi za kuchaguliwa umeanza kuzua kizaazaa nchini Brazili huku karibu watu milioni 2 wakitia saini zao kama ishara ya kuunga mkono.
Nchi za Balkani: Ufanano Baina ya Facebook na Chama cha Kikomunisti cha Yugoslavia
Filip Stojanovski anatafsiri orodha ya vitu vinavyofanan kati ya Facebook na Chama cha kikomunisti cha Yugoslavia (CPY).
Moroko: Je, Wakristu Wako Hatarini?
Mapema mwezi Machi mwaka huu, watazamaji walishuhudia jumla ya wafanyakazi wa muda mrefu katika kituo cha Kikristo cha kulelea watoto yatima wapatao 20 wakifukuzwa kutoka katika nchi ambayo wanaiona kama nyumbani. Tukio hilo pamoja na mengine kadhaa yaliyofuatia yamezusha mjadala kuhusiana na imani ya Kikristu katika ufalme huo.
Urusi: Habari za Mwanzo za Milipuko ya Mabomu
Utaratibu wa Jumatatu asubuhi mjini Moscow ulivunjwa leo na milipuko ya mabomu mawili mabomu ya kujiua, ambayo yaliua watu wapatao 38 na kujeruhi kwa uchache watu wapatao 70. Alexey Sidorenko anatafsiri baadhi ya taarifa za mwanzo kutoka katika ulimwengu blogu za Urusi.
Chile: Mchakato wa Ujenzi Mpya Baada ya Tetemeko la Ardhi
Mwezi mmoja baada ya tetemeko baya kabisa nchini Chile, Rais Sebastián Piñera ametangaza mpango wa ujenzi mpya wa miundombingu ya nchi na majengo, akiwataka raia wa Chile kutoa mapendekezo jinsi gani mchakato huo utekelezwe na kusimamiwa.