Kuna kundi la raia wa Cape Verde ambalo huandaa mikutano mjini Lisbon ili kujadili uhusiano kati ya vijana na siasa, kama anavyoeleza Suzano Costa katika video [pt] kama ilivyowekwa tena na Amilcar Tavares. Katika blogu yao – Tertúlia Crioula [pt] - unaweza kusoma maelezo yaliyochukuliwa kutoka “Cape Verde katika Mdahalo” kadhalika unaweza kusoma majadiliano mengine kuhusu masuala muhimu.
Habari Maalum Kuhusu Migration & Immigration
Kocha wa Timu ya Taifa ya Zambia Atunukiwa Ukaazi wa Kudumu

Zambia imewahi kuwa na makocha wengi wa kigeni wa timu ya Taifa ya soka, lakini ni Mfaransa Herve Renard, aliyeongoza timu hiyo hadi kushina Kombe la Washindi Barani Afrika mwaka 2012, aliyepata upendeleo wa pekee. Ili kutambua mafanikio yake haya, serikali imemtunuku ukaazi wa kudumu lakini uamuzi huo unaonekana kuwekewa chumvi ya kisiasa.
-
Dondoo za Video: Maandamano, Chaguzi, Utamaduni na GV
31 Disemba 2011
-
Côte d'Ivoire: Gbagbo agoma, Waafrika waandamana
12 Aprili 2011
-
Gabon: Wanafunzi Waandamana, Wanajeshi Wasambazwa
13 Februari 2011
-
Haiti: Pesa Zinazotumwa na Ndugu na Jamaa Zasaidia Kabla ya Misaada Rasmi 3 Februari 2010
-
Senegal Yatoa Ardhi ya Bure kwa Walionusurika na Tetemeko la Ardhi
18 Januari 2010
Habari mpya Kuhusu Migration & Immigration
7 Julai 2012
Cuba: Maandamano yafanyika Mara Mbili, Wengi Wakamatwa
Kikundi cha wanawake kijiitacho ‘wanawake wavaliao mavazi meupe’ (Ladies in White) kwa mara nyingine wametawala fikra za wanablogu wa Cuba waishio nje ya nchi. Maandamano ya amani ya kikundi hicho ambacho ni moja wapo ya vyombo vya upinzani vinavyoheshimika zaidi katika visiwa hivyo –pamoja na kukamatwa kwao mara kwa mara na vyombo vya dola –yanaendelea kuvuta hisia za watu. Mapambano ya hivi karibuni yalitokea mwishoni mwa juma lililopita wakati wanachama wa kikundi hicho walipojaribu kufanya maandamano mara mbili mjini Havana.
4 Januari 2012
Suluhisho la Kiradikali la Umaskini Duniani: Ufunguzi wa Mipaka
Wataalamu kadhaa wanasema kuwa umaskini uliokithiri hauepukiki. Suluhisho la kiradikali zaidi la kupunguza umaskini kwa haraka duniani kwa wataalamu wengi wa uchumi ni kufungua mipaka kati ya nchi na kuruhusu wafanyakazi kuhamia sehemu ambazo nguvukazi inahitajika zaidi.
27 Julai 2010
Palestina: Mateso ya Kuwa Uhamishoni
Wakimbizi wa Kipalestina ni miongoni mwa watu ambao wamejikuta wakikimbilia uhamishoni ulimwenguni kote, Umoja wa Mataifa unatoa msaada kwa jumla ya wakimbizi waliosajiliwa wapatao milioni 4.7 katika ukanda unaokaliwa kwa nguvu huko Palestina, Jordan, Lebanoni na Syria. Mamilioni ya wakimbizi wa Kipalestina na wale walioteguliwa kutoka kwenye makazi yao wanaishi sehemu mbalimbali duniani. However, their Hata hivyo, watu hawa daima mioyo yao ipo nyumbani kwao, au kwa wazazi au mababu na mabibi zao waliobaki nyuma. Wanablogu wawili wa huko Gaza wameandika kuhusu mateso ya kuwa uhamishoni.
21 Machi 2010

Lebanoni: Wafanyakazi wa Ndani Wanaotoroka
“Mfanyakazi wa ndani anapotoroka kutoka kwenye nyumba ya mwajiri wake, kituo cha polisi hakiwezi kufanya lolote kwa sababu hakuna sheria dhidi ya wafanyakazi wa ndani wanaotoroka. Kwa hiyo ofisa wa kituo cha polisi anamwambia mwajiri wa ki-Lebanoni aseme kuwa (mtoro huyo) aliiba pesa,” anaandika Ethiopian Suicides.
14 Januari 2010
Haiti: Madhira ya Tetemeko la Ardhi
Mpaka sasa taarifa za majeruhi wanaotokana na tetemeko la ardhi lililoikumba Haiti zimejikita kwenye takwimu za kutisha, lakini ni majina machache tu ndiyo yameambatanishwa kwenye namba hizo. Katika makala hii tunapata simulizi za wale walionusurika kutoka kwenye janga hili la asili kama wanavyozirusha kwenye mtandao.
13 Januari 2010

Haiti: Maoni ya Mwanzo Kuhusu Tetemeko la Ardhi Lenye Ukubwa wa 7.0
Posti ya kwanza ya blogu iliyoandikwa kwa lugha ya Kifaransa kuhusu tetemeko la ardhi huko Haiti imetokea nje ya nchi hiyo, ikitangaza habari mbaya za kuanguka kwa Kasri ya Rais, hospitali na majengo mengine na pia tishio la tsunami. Kwa mujibu wa MetropoleHaiti, Marekani tayari imekwishapendekeza misaada ya kibinadamu.
6 Januari 2010
Kuchapisha Bloguni kuhusu Utamaduni na Ndoa za Watu wa Asili Tofauti
Idadi kadhaa ya familia zinazoundwa na watu wa rangi na dini tofauti wanasimulia kuhusu uzoefu wa maisha yao katika familia zao kupitia ulimwengu wa blogu. Majaribu na mahangaiko ya wanandoa wenye asili tofauti yanaonyesha, kama kioo, jinsi sisi, kama watu tuliostaarabika, tulivyotoka mbali na hasa katika kupokea na kuheshimu tofauti zetu.
16 Novemba 2009

Karibea: Tuzo za Fasihi ya Kifaransa
Wiki hii, waandishi wawili wenye asili ya Kiafrika wanaoandika kwa Kifaransa walipewa tuzo mbili zenye kuheshimika sana katika fasihi ya Kifaransa: Ulimwengu wa blogu za wanaozungumza Kifaransa katika Karibea umekuwa ukinguruma juu ya kutosheka kwao mara mbili kwa mpigo, katika makala hii kutoka Haiti, na hii kutoka Guadeloupe na hii kutoka Martinique [Fr].
24 Oktoba 2009

China: Maisha ya Raia wa Kigeni Katika Jela ya Beijing
Raia wa kigeni ambaye alitumia muda wa miezi saba iliyopita katika jela ya Beijing No. 1 Detention Center aliitumia idhaa ya DANWEI maelezo ya kina ya maisha yake ya kila siku katika jela hiyo.




























Kiungo cha RSS kwa Migration & Immigration 










mambo vipi wanablog muko powa wote.kama mumenisoma nijibuni.
Asante. Nimepita hapa natafuta japan na china wamemalizaje ugomvi wao kuhusu visiwa,pia chanzo cha ugomvi...