The Global Voices Lingua project hopes to bring GV content to new linguistic audiences - Details

Also in:

Media Hifadhi ya mada

Kiungo cha RSS kwa Media

2009-11-05

Sub-Saharan Africa

Marvin anaandika kuhusu Afripot, tovuti ya habari inayotilia makini habari za Afrika: “Hivi sasa anatambulisha chungu cha kuyeyushia Afrika – Afripot. Tayari nimo ndani ninayeyuka na ninatumaini kukuona pale na wewe pia kwani mazungumzo kuhusu Afrika na Waafrika yanachukua kasi na kupamba moto. Ni nani ajuaye, inaweza kutengeneza joto la kutosha na kulazimisha mabadiliko tuayoyahitaji sana.”

2009-11-03

Saudia Arabia: Ambako Kuiga Kazi Kinyume cha Haki Miliki ni Kosa la Jinai

Wanablogu wa Kisaudia wanaungana ili kumuunga mkono mwanablogu mwenzao anayelituhumu gazeti moja kuwa limetumia picha na kuzinakili kutoka mwenye blogu yake bila ruhusa.

2009-10-17

Sub-Saharan Africa

Mradi Wa Uchaguzi Afrika (AEP) www.africanelections.org utakuwa unafuatilia uchaguzi mkuu wa wa 10 wa Botswana, unaofanyika Oktoba 16, 2009.

2009-07-24

Nchi za Kiarabu: Homa ya Mafua ya Nguruwe Yaendelea

Homa ya mafua ya nguruwe au H1N1 bado inatawala vichwa vya habari vya magazeti katika nchi za Kiarabu kwani wagonjwa wapya wanaendelea kugunduliwa na mamlaka za afya na kutangazwa katika vyombo vya habari kila siku. Huu ni muhtasari wa yale wanayoongea wanablogu huko Bahrain, Jordan, Misri na Syria.

2009-06-09

Uganda: Mradi wa Katine Wawafikisha Wanakijiji Kwenye Ulimwengu wa Blogu

Inakadiriwa kuwa matumizi na uenezi wa intaneti nchini Uganda ni kwa kiwango cha asilimia sita tu, idadi ambayo inazuia sehemu kubwa ya watu kujiunga na ulimwengu wa blogu nchini Uganda au kuweza kuwasiliana na ulimwengu wa blogu duniani. Mradi wa Katine unaoendeshwa na Guardian and Observer unafanya kazi kubadilisha hali hiyo katika kijiji kimoja.

2009-05-29

Uchaguzi Malawi: Utabiri wa Wataalamu wa Mambo Wageuka Batili

Wakati uchaguzi umekwisha na rais aliye madarakani Bingu wa Mutharika ameshaapishwa kwa muhula wake wa pili na wa mwisho, wanablogu wa Malawi (mabloga) bado wanashangaa kuona maendeleo kinyume na utabiri wa wengi, haswa ule watalaamu wa mambo. Utabiri wa kwanza ulikuwa kwamba ushindani ungelikuwa wa karibu sana. Haukuwa. Pili kulikuwa ...

2009-04-22

Jamhuri Ya Kidemokrasi ya Kongo: Mahojiano na Kabila Yaamsha Gadhabu

Wanablogu wa Kikongo wakosoa mahojiano ya hivi karibuni ya rais Joseph Kabila aliyoyafanya kwenye gazeti la New York times, wanauchambua msimamo wa Kabila juu ya Rwanda, ni nani wa kulaumiwa kuhusu rushwa, na jinsi wanahabari wa Magharibi wanavyoripoti kuhusu Afrika.

2009-02-26

Martinique: Uhuru na “Ubeberu” wa Kifaransa

Wakati harakati za wafanyakazi zinaendelea huko Martinique na Guadeloupe, wanablogu wa Martinique wanapima uhuru wa Idara za Ng'ambo utamaanisha nini. Le blog de [moi] anaona dhana ya kuwa Martinique haiwezi kujitegemea ni dhana inayotusi na ya kibeberu. Wasomaji wake wanadhani kuwa ukweli wa kisiwa chochote kidogo ni kuwa kila siku kitakuwa katika kivuli cha wengine.