Habari kuhusu Vyombo na Uandishi wa Habari kutoka Januari, 2010
Haiti: Kituo Cha Habari Chazinduliwa Kwa Ajili Ya Uanahabari wa Haiti
Réseau Citadelle anatangaza kuzinduliwa kwa Kituo Cha Habari, mradi unaotoka kwa Wanahabari Wasio Na Mipaka pamoja na Quebecor, wenye lengo la kuwezesha kazi za wanahabari wa ndani na wa nje ambao wako nchini Haiti, na pia kuunda ubia kati ya Asasi Zisizo za Kiserikali na Vyombo vya Habari.
China: Tangazo la Google Kusahihisha Uvumi Limezua Utabiri Mwingine
Tangazo la hivi karibuni la Google.cn linasema kuwa uvumi kuhusu kujitoa kwake ni uvumi tu. Hata hivyo, utabiri zaidi ulijitokeza, ukiuliza iwapo uamuzi wa Google unalenga kuficha kushindwa kwake kibiashara, au unalenga kutumikia maslahi ya kisiasa.
Haiti: Uenezaji Habari na Taarifa
Sisi tulio nje ya Haiti tunaweza tu kujenga picha kichwani kuhusu hali halisi ya maisha ya kila siku yalivyo huko baada ya tetemeko baya la ardhi - lakini katikati ya juhudi za kuwatafuta wapendwa ndugu, juhudi za kuwahudumia waliojeruhiwa na jukumu zito na gumu la kuwafikishia msaada wa kiutu wale wanaouhitaji zaidi - wanablogu walio huko Port-au-Prince na maeneo ya jirani wanawasiliana na ulimwengu wa nje, ambao nao unahangaika kutaka kupata taarifa kutoka kwa wale waliokuwa katika eneo lenyewe kabisa la janga.
Haiti: Madhira ya Tetemeko la Ardhi
Mpaka sasa taarifa za majeruhi wanaotokana na tetemeko la ardhi lililoikumba Haiti zimejikita kwenye takwimu za kutisha, lakini ni majina machache tu ndiyo yameambatanishwa kwenye namba hizo. Katika makala hii tunapata simulizi za wale walionusurika kutoka kwenye janga hili la asili kama wanavyozirusha kwenye mtandao.
Thailand: “Tumechoshwa na Wizara ya Utamaduni”
Ukurasa wa wapenzi wa Facebook umezinduliwa na raia wa mtandaoni wanaokosa njia na sera za Wizara ya Utamaduni ya Thailand. Wizara hiyo imekuwa ikidhibiti sana uhamasishaji na usimamizi wa utamaduni wa asili wa Ki-Thai katika tovuti za vyombo vya habari vya kizamani na hata vile vya kisasa.
Georgia: Hebu Tuongelee Tendo la Ngono…
Pengine mada iliyotawala katika vyombo vya uanahabari wa kijamii vya Georgia haikuwa siasa, uchaguzi, matatizo, matetemeko ya ardhi au majanga. Badala yake, mada iliyojadiliwa sana ilikuwa inahusu kipindi kipya cha televisheni, Ghame Shorenastan. Kinachoonyeshwa kwenye Imedi TV, jina la kipindi hicho linatafsirika kama Usiku pamoja na Shorena na kinaongelea mada zinazohusu tendo la ngono.
Japan: Tangaza Ujumbe, Tafsiri
Mahojiano ya video [en] ya Kyo Kageura, mkuu wa mradi wa Minna no Honyaku (みんなの翻訳, Tafsiri kwa Wote) [ja], jukwaa jipya la tafsiri ambalo linazisaidia Asasi Zisizo za Kiserikali na zile Zisizo za Kibiashara kueneza ujumbe wao, shukrani kwa wafasiri wa kujitolea. Global Voices Japan ilimuuliza kuhusu changamoto za Minna...