GlobalVoices katika

Media & Journalism

Hifadhi ya mada · 80 jumbe


Habari mpya Kuhusu Media & Journalism

28 Januari 2013

Mauritania:Ghadhabu Dhidi ya Kauli ya Balozi wa Marekani

Picha ya maandamano dhidi ya Ubalozi wa Marekani mjini Nouakchott – Iliwekwa kwenye ukurasa wa Facebook ya Vijana wa Kukusanya Nguvu ya Kidemokrasia

zaidi »

27 Disemba 2012

Maisha Binafsi ya Watawala Wapya wa China

Shirika la Habari la Xinhua lilichapisha[zh] mfululizo wa wasifu wa maisha binafsi ya watawala wa juu China, ikiwa ni pamoja na picha za familia zao, ambazo ni nadra sana katika vyombo vya habari vya China. Hatua hiyo imechukuliwa na wengi kama dalili nyingine kuwa utawala mpya wa China unaweza ukawa na namna mpya ya utawala inayotofautiana na waliopita. Offbeat China wana habari za kina zaidi.

23 Disemba 2012

Utambulisho wa Jamii ndogo ya Balkan

Face the Balkans subjects of stories

Picha ya mwonekano wa tovuti ya Balkans.

Waandishi vijana kumi na watano kutoka katika nchi zipatazo sita tofauti wametengeneza mfululizo wa masimulizi binafsi kuhusu masuala ya namna jamii zenye watu wachache (kwa mapana yake) zinavyoweza kuwakilishwa kutoka Bosnia na Herzegovina, Kosovo, Serbia, na Macedonia. Habari zinapatikana katika lugha za Kiingereza, Kijerumani, na Kifaransa katika mwonekano wa tovuti ya Balkans.

15 Oktoba 2012

China: Hatua za Kubana Uhuru wa Habari Majimboni

Jing Gao kutoka blogu ya Tofu anaeleza namna serikali ya Fuji ilivyo na mikakati michafu dhidi ya Yunnan na jinsi inavyochukua hatua za kuzuia uchapishaji wa habari zinazoweka wazi kashfa za ufisadi zinazomkabili afisa mmoja wa serikali.

19 Septemba 2012

Je, Sifa ya ‘Kisiwa cha Amani’ Tanzania Imeanza Kutoweka?

Soma makala hii.

Tanzania imeshuhudia matukio kadhaa mabaya tangu kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa 2010. Tukio la hivi karibuni ni kifo cha kikatili cha mwandishi wa habari wa Tanzania Daudi Mwangosi, aliyeuawa kwa bomu la machozi huko Iringa, Kusini mwa Tanzania, wakati polisi walipojaribu kukitawanya kikundi cha wafuasi wa chama cha upinzani.

16 Septemba 2012

Global Voices Yashinda Tuzo Ya Highway Africa

Highway Africa Award for Global Voices

Washindi: Dorothee Danedjo kutoka Kameruni akiwa na Ndesanjo Macha wa Global Voices. Picha ya Ettione Ferreira (imetumiwa kwa ruhusa)


Timu ya Global Voices inayoandika habari za Nchi za Afrika zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara imeshinda Tuzo ya Telekom Highway Africa katika kundi la “Blogu bora ya TEHAMA ya Kiafrika”. Mhariri wa Eneo hilo Ndesanjo Macha alikuwepo Afrika Kusini kuipokea tuzo hiyo (na kikombe cha ushindi!) tarehe 11 Sepetemba, 2012 kwa niaba ya timu nzima. Mwanablogu na mwandishi wa habari Dorothy Dandejo kutoka Kameruni alikuwa mshindani wa karibu aliyeibuka mshindi wa pili katika kundi hilo hilo.

27 Agosti 2012

Mgogoro wa Umoja wa Ulaya: Kitabu cha Kwanza cha Global Voices cha Kieletroni

Soma makala hii.

"Umoja wa Ulaya katika Mgogoro" (EU in Crisis) ni chapisho letu la kwanza katika Mradi wa Vitabu wa Global Voices na ambao unahusisha makala bora zaidi kuhusu mazungumzo ya kijamii, ushiriki na uhamasishaji unaopewa nguvu na raia wanaopitia nyakati ngumu za kubana matumizi katika bara la kale zaidi na kwingineko.

31 Julai 2012

Angola: Raia Wadai Kampeni za Uchaguzi za Wazi

Asasi za kiraia nchini Angola zinatoa wito wa uwazi zaidi [pt] katika maandalizi ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika tarehe 31 agosti, 2012. Moja wapo ya miradi iliyozinduliwa hivi karibuni kwa lengo hilo ni maombi ya mtandaoni [pt] ikiwataka viongozi wa vyama vinavyoshiriki uchaguzi huo kushiriki midahalo ya moja kwa moja kupitia televisheni za nchi hiyo.

30 Julai 2012

Tanzania: Kufungiwa ‘Mwanahalisi', uhuru wa habari mashakani?

Mnamo tarehe 30 Julai, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Msajiri wa Habari ilitangaza kulifungia kwa muda usiojulikana gazeti la Kiswahili linalotoka mara moja kila wiki la 'MwanaHalisi'. Ulimwengu wa habari umepokea taarifa hiyo kwa mshtuko mkubwa. Hivi ndivyo wanaharakati wa mtandaoni wanavyoeleza hisia zao kuhusu tangazo hilo.

15 Julai 2012

Afrika: Ujuzi wa Matumizi ya Zana za Habari za Kijamii kwa Vijana Wanaoishi na Ulemavu.

Soma makala hii.

Warsha ya vijana walemavu kutoka kote barani Afrika lafanyika Dakar, Senegali. Warsha hii ilipangwa na DRI na YI. Imeandikiwa na Haute Haiku.

Sehemu za Dunia

Nchi

Lugha