Habari kuhusu Lugha
Shiriki Zoezi la Kujifunza Lugha za Asili Mtandaoni
Badala ya zoezi la kuweka mabonge ya barafu vichwani mwao, watetezi hawa wa lugha wamekubali kushiriki zoezi la lugha za asili kwa njia ya video
Hivi Ndivyo Waandishi wa Kifaransa wa Global Voices Wajivyojipanga Kusoma Kiangazi Hiki
Je, unahitaji kitabu cha kujisomea? Hapa kuna orodha ya kusoma iliyopendekezwa na waandishi wa Kifaransa kwa familia ya GV.
Namna Teknolojia Inavyosaidia Watu Kujifunza —na Hata Kuokoa—Lugha za Dunia
Waleta mabadiliko sasa wanatumia nguvu ya teknolojia kujaribu kuziokoa lugha zilizo kwenye hatari ya kupotea, na kwa nadra, kuzifufua lugha zilizokwisha kufa.
Maneno Yasiyotafsirika Yafafanuliwa kwa Michoro
Tovuti ya Pijamasurf [es] inazungumzia “orodha ya maneno 30 yasiyotafsirika” ambayo msanii mchunguzi Anjana Iyer [en] alijaribu kuyachorea mchoro wenye kuchekesha kidogo. Kwa mfano: Bakku- shan (Kijapani) Msichana mzuri…almuradi tu anaangaliwa kutokea nyuma. Unaweza kuipata orodha hiyo hapa.
Maandamano ya Taiwan ya #KupingaBunge, Yatafsiriwa
Mamia ya watafsiri wamejipanga kupitia mtandao wa facebook kutafsiri habari kuhusu maandamano ya raia wanaojikusanya kwenye Bunge la nchi hiyo kupinga hatua ya chama tawala nchini humo kupitisha mkataba wa kibiashara wenye utata na nchi ya China.
Flipboard Yaiongeza Global Voices Kwenye Mwongozo wake wa Maudhui
Kuanzia mwezi huu, mtandao wa Global Voices (katika lugha tofauti) utakuwa ukipendekezwa kwa maelfu ya watu wanaotumia simu ama vifaa vinavyofanana na simu za kisasa.
Global Voices Yaanzisha Ushirikiano na Shirika la Kukutanisha Wakimbizi
We're proud to assist Refugees United with translation and local advice as they help families who have lost each other reconnect online.
Honduras Yazindua Kamusi ya Mtandaoni ya Lugha za Asili
Kamusi ya lugha za asili nchini Honduras ilisambazwa mtandaoni hivi karibuni[es]. Gazeti la Honduras liitwalo Tiempo [es] linaeleza kuwa kamusi hii “imejumuisha maneno yanayofanana katika lugha ya Kihispaniola, chortí, garífuna, isleño, miskito, pech, tawahka na tolupán, lugha ambazo ndizo zinazotengeneza urithi wa lugha wa nchi hiyo.” Kwa mfano, unapotafuta neno...
Orodha ya Waliouawa Katika Maandamano ya Venezuela Yapatikana kwa Lugha Tano
Katika blogu ya Panfleto Negro [es], John Manuel Silva na Emiliana Duarte wanafuatilia orodha ya vifo vilivyotokea kufuatia maandamano yanayoendelea nchini Venezuela. Orodha hiyo -ambayo awali ilikuwa kwa lugha ya Kihispania-imetafsiriwa kwenda lugha ya Kiingereza, Kijerumani, Kiitaliano/a> na Kifaransa.
Wikipedia kwa Lugha ya Ki-Guarani
Mwaka huu, Wikipedia katika lugha ya Kihispaniola ilifikia makala milioni moja na kutolewa kwa mwongozo msingi wa mtumiaji katika lugha ya ki-Guarani. Wazo ni kufufua jamii ya wanaozungumza kiguarani katika jukwaa hili kubwa. Hadi sasa kuna makala 20 tu katika lugha hiyo. […] Kama una nia ya kushirikiana na mradi...