Habari kuhusu Lugha kutoka Februari, 2014
Honduras Yazindua Kamusi ya Mtandaoni ya Lugha za Asili
Kamusi ya lugha za asili nchini Honduras ilisambazwa mtandaoni hivi karibuni[es]. Gazeti la Honduras liitwalo Tiempo [es] linaeleza kuwa kamusi hii “imejumuisha maneno yanayofanana katika lugha ya Kihispaniola, chortí, garífuna, isleño, miskito, pech, tawahka na tolupán, lugha ambazo ndizo zinazotengeneza urithi wa lugha wa nchi hiyo.” Kwa mfano, unapotafuta neno...
Orodha ya Waliouawa Katika Maandamano ya Venezuela Yapatikana kwa Lugha Tano
Katika blogu ya Panfleto Negro [es], John Manuel Silva na Emiliana Duarte wanafuatilia orodha ya vifo vilivyotokea kufuatia maandamano yanayoendelea nchini Venezuela. Orodha hiyo -ambayo awali ilikuwa kwa lugha ya Kihispania-imetafsiriwa kwenda lugha ya Kiingereza, Kijerumani, Kiitaliano/a> na Kifaransa.