Mradi wa Lingua wa Global Voices katika lugha ya ki-Malagasi umechapisha mtandaoni posti yake ya 5,000. Mradi huo ulianza mwezi Septemba 12, 2007 ukiwa kati ya miradi ya mwanzo kabisa ya Mradi mkubwa wa Lugha za Kiafrika. Kwa sasa mradi huo unaendeshwa na watafsiri wa ki-Malagasi wapatao 16 miongoni mwao akiwamo mmoja wa watafsiri wadogo kabisa wa Global Voices , mwenye umri wa miaka 16 aitwaye Radifera Felana Candy.
Habari mpya Kuhusu Language
27 Agosti 2012
Mfumo wa Kipekee wa Kuwapa watoto Majina wa Nchini Myanmar (Burma).
Raia wengi wa Myanmar hawana majina ya ukoo. Je, umewahi kujiuliza wanajaza vipi fomu zinazowadai kujaza majina yao ya mwanzo na ya ukoo, au hata kujiuliza kuwa 'Daw' ina maana gani katika jina la Daw Aung San Suu Kyi? Hapa tutatazama mtindo wa pekee kabisa wa Mynmar wa kutoa majina.
30 Aprili 2012
Ajentina: Dokumentari Kuhusu Wenyeji wa Mjini Yatafuta Tafsiri ya Maandishi
Dokumentari iitwayo Runa Kuti iliyoshirikishwa katika mradi wa Haki miliki wa “Creative Commons” kuhusu kutambuliwa kwa wananchi waliotokana na uzao wa wenyeji wa zamani walioishi mjini katika jiji la Buenos Aires, inatafuta watu wa kujitolea kusaidia kuiwekea video hiyo tafsiri ya maandishi kwenda katika lugha za asili za Ajentina kama ki-Quechua, ki-Aymara, -kiMapuche na ki-Guaraní pamoja na ki-Kiingereza.
9 Septemba 2010
Africa: Waafrika Wasimulia Kumbukumbu Zao za Utotoni
That African Girl ni blogu yenye mfululizo wa makala zilizoandikwa na Waafrika kutoka dunia nzima kuhusu maisha ya utotoni. Ni blogu inayoelezea kuhusu makuzi katika familia za Kiafrika na uzoefu wa kuishi katika tamaduni mbili.
7 Aprili 2010
Tunisia: Wanablogu wa Tunisia Wazungumza Kiingereza
Wanablogu wa Tunisia walizoea kuepuka kutumia Kiingereza (lugha ya tatu nchini mwao), na badala yake waliandika kwa Kiarabu (na wakati mwingine kwa lahaja za Tunisia) au Kifaransa. Lina Ben Mhenni anazitupia macho baadhi ya blogu zinazoandikwa kwa lugha ya Kiingereza.
22 Januari 2010

Kenya: Kiswahili Kuwa Somo La Kuchagua
Bunmi anaandika kuhusu uamuzi wa kulifanya somo la Kiswahili kuwa la kuchagua nchini Kenya: “Somo hili halitakuwa tena na mtihani wa lazima katika mtihani wa taifa wa darasa la nane…”
6 Januari 2010
Slovakia, Hungaria: Heri ya Mwaka Mpya!
Uhusiano kati ya nchi mbili jirani za Slovakia na Hungaria ulianza kutetereka katika mwaka uliopita - lakini baadhi ya wananchi wa Slovakia na Hungaria wanafanya juhudi kurekebisha hali hiyo kwa kuzindua kampeni ya mtandaoni inayojulikana kama "Štastný nový rok, Slovensko! / Boldog Új Évet Magyarország!" ("Heri ya Mwaka Mpya, Slovakia!/Heri ya Mwaka Mpya, Hungaria!).
3 Januari 2010
Japan: Tangaza Ujumbe, Tafsiri
Mahojiano ya video [en] ya Kyo Kageura, mkuu wa mradi wa Minna no Honyaku (みんなの翻訳, Tafsiri kwa Wote) [ja], jukwaa jipya la tafsiri ambalo linazisaidia Asasi Zisizo za Kiserikali na...
30 Disemba 2009

Msumbiji: Je, ni Lugha Ngapi Zinazungumzwa Nchini?
Kuna lugha 20 zinazozungumzwa nchini Msumbiji, kwa mujibu wa tovuti ya serikali, zaidi ya lugha ya serikali ya Kireno. Carlos Serra [pt] anajiuliza kama kuna lugha nyingine zaidi, kwa mujibu wa wataalamu wa lugha mashuhuri:”Kuna mtu aliniambia kuwa zipo kati ya 20 na 26; mwingine akaniambia zipo 17 zilizoandikwa na nyingine bado hazijaweza kuandikwa”.
12 Disemba 2009
Twita Kutoka Beirut: Siku ya Pili ya Warsha ya Wanablogu wa Uarabuni
Siku ya pili ya Warsha ya Wanablogu wa Kiarabu ilianza na mada inayohusu Mtandao wa Herdict, tovuti inayotumia vyanzo vya watumiaji kukusanya taarifa za uchujaji wa habari kwenye intaneti kutoka...




























Kiungo cha RSS kwa Language 







mambo vipi wanablog muko powa wote.kama mumenisoma nijibuni.
Asante. Nimepita hapa natafuta japan na china wamemalizaje ugomvi wao kuhusu visiwa,pia chanzo cha ugomvi...