Habari kuhusu Habari za Wafanyakazi kutoka Oktoba, 2012
Ghana: Vikwazo Vinavyowakabili Wanawake Kimaendeleo
Betty Mould Iddrisu, Jaji na Waziri wa Sheria wa Ghana, anaandika [fr] kwenye blogu ya pambazuka.org: Kufikia ngazi za juu kabisa za utawala si rahisi, na hata unapopanda mpaka juu kabisa, bado unajikuta unakabiliwa na hisia za watu zenye uadui na watu wanakuwa na mashaka na uwezo wako, kwa sababu...
Côte d'Ivoire: Wafanyakazi wa Afya Wagoma baada Miezi Minne Bila Mshahara
S.B anatoa maoni juu ya kuanza kwa mgomo usio na ukomo unaoratibiwa na wafanyakazi wa taasisi za afya mjini Abidjan. Katika mtandao wa Connection Ivorienne, anabainisha [fr] kwamba: Kufuatia mabadiliko ya utolewaji wa huduma za afya ambazo zilitolewa bure kabisa baada tu ya kumalizika kwa mgogoro wa baada ya uchaguzi,...
Tunisia: Mgomo Waanza jijini Thala
Kupitia mtandao wa twita, Tounsia Hourra (m-Tunisia huru) anasema [ar] kuna mgomo mkubwa umeanza jijini Thala, kwenye jimbo la Kasserine, leo [Oktoba 8, 2012]. Mgomo huo umekuja kama hatua ya kupinga kukua kwa kasi kwa ukosefu wa ajira na kuzorota kwa maendeleo ya jiji hilo. @tounisiahourra: اضراب عام في تالة...