2009-07-22
Afrika: Obama Atumia Nyenzo Mpya za Habari Kuzungumza na Waafrika
“Umeshawahi kutaka kumuuliza kijana wetu wa Nyangoma maswali yoyote? Kwa maneno mengine, je ungependa Rais wa Marekani, Barack Obama ajibu maswali yako?,” ndivyo inavyoanza makala kwenye blogu ya Hot Secrets inayohusu matumizi ya Obama ya zana mpya za habari ili kukutana na kuongea na Waafrika wa kawaida.
2009-06-13
Ramani ya Ulimwengu wa Blogu za Irani Siku ya Mkesha wa Uchaguzi
John Kelly na Bruce Etling wanaelezea utafiti wao unaohusu ulimwengu wa blogu za Irani na uchaguzi katika blogu ya Intaneti na Demokrasi. Intaneti na Demokrasi ni blogu ya timu ya mradi wa Intaneti na Demokrasi wa Kituo cha Berkman cha Intaneti & Jamii kilichoko Harvard.
Kufuatana na ufuatiliaji wetu wa ...
2009-06-08
Malawi: Wasikilize wanablogu wa uchaguzi Malawi
Wamalawi wanapiga kura katika uchaguzi wa Raisi na Bunge. Baadhi ya wanablogu walipatiwa mafunzo na PenPlus Bytes, Taasisi ya kimataifa ya Uandishi wa TEKNOHAMA kwa ushirikiano na New Media Insitute kwa lengo la kuangalia na kutoa maoni yao kuhusu uchaguzi huo kwa kutumia blogu, teknolojia ya twita na simu za viganjani. Hebu na tuziangalie blogu zao, ambazo zimehifadhiwa katika Potal ya chaguzi za Afrika. Poto hii hutoa taarifa za kutosha kuhusu chaguzi mbalimbali katika nchi za kiafrika.
2009-02-04
2009-02-02
Bahrain: Mabloga Waungana Kupinga Uamuzi wa Kufungwa Kwa Tovuti
Wanablogu wa Bahrain wameujia juu uamuzi wa Waziri wa Habari wa nchi hiyo wa kuzuia upatikanaji wa tovuti mbalimbali, kadhalika kuzuia matumizi ya tovuti vivuli [proxy sites] zinazoruhusu watumiaji kuperuzi tovuti nyingine zilizozuiwa na zana za kuchuja habari. Ayesha Saldanha anaangalia maoni kutoka Bahrain.
2009-01-26
Blogu za Afrika Zapendekezwa Kupokea Tuzo ya Bloggies 2009
Blogu zilizopendekezwa kwa ajili ya Tuzo ya Tisa ya Zawadi za Weblog: Mapendekezo ya blogu katika mashindano ya Bloggies ya 2009 yalifunguliwa tarehe 1 Januari na kufungwa tarehe 19 Januari. Kwa mujibu wa waandalizi, mashindano hayo ya Bloggies ni mashindano ambayo yamedumu kwa muda mrefu zaidi mtandaoni, na mapendekezo pamoja na uchaguaji wa washindani katika fainali, ni juu ya msomaji wa blogu. Mshindi hupata senti 2,009 za Marekani! Je, ni mabloga gani wa Kiafrika waliopendekezwa kwa ajili ya kinyang'anyiro cha blogu bora zaidi?
2009-01-08
Palestina: Mawasiliano na Gaza
Katika mazingira ya kawaida bila kiwango kikubwa cha wanaojua kusoma, usambaaji wa intaneti husimama kati ya asilimia 13 mpka asilimia 15 (Gaza na Ukingo wa Magharibi kwa pamoja). Kutokana na mashambulizi yanayoendelea huko huko Gaza, uwezo wa kutumia intaneti umepungua sana. Japokuwa kuna idadi ndogo ya wanablogu wanaoandika moja kwa moja kutokea Gaza, wakazi wengine wengi wanatumia ujumbe wa maandishi wa simu za mkononi pamoja na simu nje ya nchi katika matumaini kwamba ushahidi wao utapata sehemu ya kuelezwa.
2008-11-04
Afrika ya Kusini: Matumizi ya Simu za Viganjani Kupambana na UKIMWI
Afrika ya Kusini imegundua silaha mpya katika vita dhidi ya VVU/UKIMWI - simu za viganjani. Kwenye mchakato mpya, jumbe za maandishi zitakuwa zikitumwa kila siku kuwahamasisha Wa-Afrika ya Kusini kwenda kupimwa na kutibiwa ugonjwa huo.
Mradi huo, unaoitwa Mradi wa Masiluleke au Project M, ulitangazwa rasmi wiki iliyopita wakati wa kongamano ...
2008-10-26
Misri: Sisi sote ni Laila
Sisi sote ni Laila, ndivyo wanavyosikika kusema kwa sauti moja wanablogu wa kike wa Misri. Hivi, huyu Laila ni nani na kwa nini wasichana na wanawake wa kiMisri wanapenda kufananishwa naye? Hebu endelea kusoma ili uone ni kwa namna gani wanablogu wa Misri wanavyojihangaisha ili kuvunjilia mbali vikwazo vya jinsia na kufanya sauti zao zisikike.
2008-09-12
Jordan: Ubloga wa Video wa Malkia Rania
Chombo cha habari cha Blogger Times kinachoendeshwa na mabloga wa Kiarabu, kimemtaja Malkia Rania wa Jordan kuwa bloga maarufu zaidi wa video za kutoka Uarabuni katika chombo cha Video mtandaoni, YouTube, kufuatia mafanikio ya mlolongo wa video za YouTube aliouanzisha kuondoa dhana potofu dhidi ya Waarabu.




